MAKALA MAALUMU

NI KILIO CHA WATANZANIA





TANZANIA ILIINGIA KATIKA MFUMO WA VYAMA VINGI KWA KULAZIMISHWA, KUFUATA MKUMBO AU KUFURAHISHA MATAIFA YA ULAYA KWA SERA YAO YA LIBERAL DEMOCRACY? 

Kila mtanzania anayetafakari kiuhalisia na aliyekomaa kisiasa achilia hao wanaoshangilia ka simba na yanga anashangaa saaana kuona serikali kupitia chama tawala inatumia nguvu nyingi kudhoofisha ushindi wa vyama vya upinzani bara na visiwani huku Tanzania ikiwa ni moja ya nchi iliyoridhia mfumo wa vyama vingi na uchaguzi wa kidemokracy!

Bora wangesema tukae katka mfumo wa chama kimoja kuliko kuliko kufanya unafiki eti uchaguzi wa kidemokrasia wakati ubabe, wizi wa kura, kuchakachua, kuwa na kura feki, vituo feki vikitawala hivi hiyo ndio democracy?

Kama watanzania wanaamua halafu watu wachache kupitia taasisi walizoteua wanabaka demokracy unadhani huu utawala utakuwa mnyoofu kamwe madonda ya watanxania hayatakuja futika na wataendelea kuichukia serikali iliyoingia kibabe!

Watanzania tumejifunza mengi katika uchaguzi huu ikiwemo uchu wa madaraka, hila za waziwazi, uonezi na kuminya haki lkn Mungu daima huwa hadhihakiwi! Malipo ni hapa hapa duniani!

Watanzania wanaelewa raisi wao ni Mh. Edward Ngoyai Lowasa aliyepata kura 62% za halali na wanaccm wanajua raisi wao ni Mh.John Pombe Magufuri aliyepata 58% za kupikwa na nec kupitia vituo vyao vya kuchakachua kura toka majimboni!

RAISI WA MIOYO YA WATANZANIA NO LOWASA NDIO MAANA HATA USHINDI WAKE MIJI MINGI HAUJASHANGILIWA BALI WALIOFURAHI NI HAO HAO WALIOCHAKACHUA MAANA NI WA HILA! MUNGU ATAWAADHIBU KWA DHULUMA HIYO!





KWA DALILI HIZI ZA WIZI MKUBWA YAPASA KULINDA KURA ZETU

Asalam alyekum

Kama utapata bahati au wasaa kupitia mitandao ya kijamii na kujua kinachoendelea nchi nzima kuamkia siku ya uchaguzi wa madiwani,wabunge na rais . basi hakika utakutana na hii habari iliozagaa sana na kutawala mitandao ya kijamii kwa siku mbili hizi.ni habari inayohusu kukamatwa kwa magari mawili ya serikali moja huko mkoani Njombe,gari mali ya Tanroads na jingine katika jji la Mwanza.lakini pia kule Hanang   kakamatwa mtumishi wa serikali na kada wa chama cha mapinduzi Mh Marry Nagu.
Hakika mwanzoni akili yangu haikutaka kukubaliana na mawazo ya Mh Mbowe na wenzie ya kuhamasisha  vijana wa kitanzania kukaa mita mia mbili (200) walinde haki yao ya msingi isipotee lakini dalili hizi zilizoanz akujionyesha hadharani hakika sasa natambua nini walimaanisha hawa waheshimiwa na kuunga mkono hoja hiyo.
CCM kama chama tawala na kongwe hapa nchini na Africa walipaswa wao ndio wawe kielelezo  tosha cha demokrasia ya kweli lakini pia wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuzuia viashiria vyote vya uvunjifu wa amani hii tuliochiwa na wazee wetu.ila leo hii imekua vinginevyo,chama hicho kikongwe ndio kimeanza kuonyesha rafu mbaya za uchaguzi hata kabla kura zenyewe hazijapigwa.


Nilisikia wakijitetea hawahusiki na mpango wa Mh MARRY Nagu wa kujiandalia kura za wizi ili aweze kushinda.,lakini vip hili la mkoani Njombe amabapo wananchi wamekamata gari mali ya Tanroads ( taasisi ya ujenzi wa barabara iliochini ya wizara ya ujenzi )  ambayo ni wizara inayoongozwa na Mh John P Magufuli (mgombea urais kwa tiketi ya CCM) .
GARI AINA YA LANDCRUISER STK 4599 MALI YA TANROADS LILIOKAMATWA NJOMBE LIKIWA NA KURA ZA MAGUFULI,MKOANI NJOMBE.

kilichokibaya zaidi ni wahusika waliokutwa kwenye gari hilo walipohojiwa nawakadai kuwa wanasafirisha t-shirt zenye ya mgombea huyo  lakini gari lilipokaguriwa ndipo zikakutwa na hizo kura za wizi.  Kwa mazingira haya sijui mtasema nini ambacho watanzania watawaelewa na kuwaamini kua huu ni uchaguzi huru,wahaki na amani

kuonesha dhahiri huu ni mpango wa CCM ambao pia haungwi mkono na watanzania wengi wanaopenda mabadiliko.jioni ya leo tarehe 24/10/2015 masaa machache kabla ya uchaguzi mkuu.mzigo mwingine wa kura feki umekamatwa mjini Tanga ukiwa unasafirishwa kutoka jijini D ar es salaam kwa njia ya basi
PICHA IKIONYESHA MABOKSI YA KUPIGIA KURA YENYE KURA AMBAZO ZIMEKWISHAPIGWA YALIOKAMATWA KWENYE BASI LA TAHMEED MJINI TANGA 

Gari likiteketea kwa moto baada ya wananchi wenye hasira kali  wakazi wa jiji la Mwanza kuliwasha mara punde walipojiridhisha kuwa nalo  liliku limebeba kura za wizi                                                                                                                                                                                                               

HOTUBA YA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA JANGWANI OKTOBA 24, 2015

NDUGU
Watanzania wenzangu
•       Ndugu
       wanachama, marafiki na wapenzi wa CHADEMA
•       Ndugu
        Viongozi wakuu wa kitaifa na wanachama wa vyama vyetu vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
•       Ndugu
        Wana mabadiliko na watetezi wa kweli wa maendeleo
•       Mabibi kwa Mabwana


Salaam Aleikum

Bwana Yesu Asifiwe

Tumsifu Yesu Kristo

NIANZE hotuba yangu hii ya kuhitimisha ziara ndefu za kampeni, zilizonichukua mimi na timu yetu yote ya kampeni katika kaya, vijiji, kata, tarafa, wilaya na mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar katika kipindi chote cha siku takriban 60.

Kama nilivyosema jana nilipozungumza na Watanzania kupitia katika redio, televisheni na kwa njia tofauti za mawasiliano, tuna kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema aliyetuvusha salama.

Leo tunahitimisha safari ngumu, ndefu, iliyojaa miiba, milima na mabonde tukitembea kifua mbele kwa namna mamilioni ya Watanzania walivyojitokeza kutuunga mkono.

Kwa uchungu na masikitiko makubwa tunahitimisha safari ya kampeni, tukiwa na kumbukumbu mbichi vichwani ya kuwapoteza wenzetu kadhaa.

Ni juzi tu, wiki hii hii tumemlaza katika nyumba yake ya milele Mzee wetu, Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Emmanuel Makaidi.

Tumewapoteza njiani kabla yake, Deo Filikunjombe, Dk. Abdallah Kigoda, Mama Celina Kombani, kijana wetu Mohamed Mtoi na Estom Mallah, wote hawa walikuwa wagombea ubunge.

Si hao tu, tukampoteza pia mmoja wa wanasiasa ambaye ni muasisi wa mageuzi nchini, Mwenyekiti wa chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila.

Wote hao na wengine ambao sikuwataja hapa tunamuomba Mwenyezi Mungu awapumzishe kwa amani. (Tusimame dakika moja kuwakumbuka marehemu wote waliopoteza maisha katika kipindi hiki cha kampeni)




Ndugu zangu
               
        Mimi na mgombea mwenza, Juma Haji Duni tumeona na kujifunza mengi. Tumejiandaa kikamilifu kuijenga Tanzania Mpya. Tanzania ya ndoto ya waasisi wetu.
Ndugu Watanzania wenzangu
Katika ziara hizi, nimeshuhudia vuguvugu la mabadiliko, kiu na ari ya Watanzania kuyapokea mabadiliko hayo.
Lakini pia nimejionea shida zinazowakabili wananchi hao.
Nimesikia na nyakati nyingine kujionea kilio chao cha kunyanyaswa na kunyimwa haki zao na watendaji wa serikali na baadhi ya vyombo vya dola.
Nimekisikia kilio chao cha umaskini, afya na elimu duni.
Nimekisikia kilio kikubwa cha vijana kukosa ajira na matarajio ya kesho bora.
Nimesikia rai za Watanzania na ndoto zao za kupata maendeleo, maji safi, makazi bora na barabara madhubuti.
Nimesikia malalamiko ya wakulima na wafugaji kukosa maji, ardhi na namna wanavyotozwa ushuru na kodi za kero katika mazao yao.
Nimesikia kilio cha madaktari, wauguzi, walimu, askari na watumishi wa taasisi za umma kuhusu mazingira magumu ya kazi, kodi za juu na maslahi duni.
Nimesikia kilio cha wafanyabiashara wadogo wadogo kuhusu ugumu wa mazingira ya kufanyia shughuli zao, kodi kandamizi na kukosa mitaji.

Nimesikia kilio cha wanawake kuhusu haki zao na ushiriki wao mdogo katika shughuli za kiuchumi.

Nimesikia kilio cha wazee na wastaafu wasio na bima ya afya, wanaolipwa pensheni isiyokidhi mahitaji yao na ugumu wa maisha yao uzeeni.
Tumekisikia kilio dhidi ya rushwa na ufisadi uliokithiri
Tumekisikia kilicho cha Watanzania juu ya udhaifu wa kiuongozi na utawala dhaifu wa CCM ulioshindwa kuondoa umaskini
Tumekutana na vilio vya watu walioonewa, kunyanyaswa na kupuuzwa na namna haki za raia zilivyopuuzwa.
Jibu langu ni fupi na lile lile. TUMEONA, TUMESIKIA, TUMEELEWA NA TUTATENDA.

        Baba wa Taifa, alisema Uongozi ni kuonyesha njia. Tumejipanga vyema kuwaongoza Watanzania:

        •       Kwanza tumejiandaa kuongoza mapambano ya dhati ya kuukataa na kuondokana na umaskini

        •       Tumejipanga vyema kupiga vita rushwa na ufisadi kwa matendo na si kwa maneno matupu

        •       Tumejizatiti kuliandaa taifa kwa ajili ya mapinduzi ya kweli katika elimu, kilimo, viwanda

        •       Tumejiandaa vyema kuwaongoza Watanzania kuachana na mawazo ya kutegemea wafadhili na kuondokana na hulka za kuwa taifa ombaomba

        •       Tumejipanga kufufua ari, dhamira na misingi ya kujenga taifa linalojitegemea kiuchumi.

        •       Tumejiandaa vilivyo kuhakikisha tatizo sugu la ajira linakoma.

        •       Tumeshaanza kufanya maandalizi ya kuhakikisha serikali tutakayoiunda itafungua fursa mpya za ajira za ndani na nje ya nchi kwa vijana wa Kitanzania

        •       Tumejizatiti kisera na kimikakati kuwajengea Watanzania misingi na utayari wa kujiamini kifikra na kuchochea fikra za kizalendo

        •       Tumejipanga na kujizatiti vyema kuleta mabadiliko na mapinduzi katika utendaji wa kazi serikalini

        •       Tumejiandaa vyema kuijenga na kuiimarisha sekta binafsi na kuijengea mazingira bora ya ushindani

        •       Tumejiandaa vyema kubadili na kuboresha maisha ya wajasiriamali wadogo kama wamachinga, bodaboda na mama ntilie wakue na kukomaa kibiashara.

        •       Tumejipanga vyema kuhakikisha raslimali za taifa tulizonazo kama madini, gesi asilia na vivutio vya utalii vinaimarishwa na kuwanufaisha Watanzania kwanza na siyo wageni kama ilivyo sasa.




        •       Tumejizatiti kuifanya Tanzania kuwa taifa la mfano kijamii, kiuchumi na kimaendeleo Afrika Mashariki na duniani kwa kudumisha sera yetu ya uhusiano wa kimataifa ili iwe na tija kwa Watanzania.

        •       Tumejiandaa kuiondoa Tanzania kutoka katika kundi la mataifa maskini duniani kwa kuhakikisha tunaanza kutumia vyema raslimali zetu kujiletea maendeleo ya dhati.


Mambo hayo ndiyo msingi wa dhana ya mabadiliko tunayoyataka na kuyahubiri.

Tunaamini na kutambua kwamba, mabadiliko yanaanza na fikra.

Sisi wana mabadiliko tunaamini kwa dhati kwamba MAENDELEO NI AJENDA YA DHARURA kwa taifa na siyo jambo la lelemama.

Nimepata kulisema hilo siku zilizopita na nalisema tena leo kwamba, serikali nitakayoiongoza itaanzisha mchakato mahususi wa MCHAKAMCHAKA WA MAENDELEO.

Ni kwa sababu hizo, nawaomba Watanzania watuamini na wakubali kutupa dhamana ya kuliongoza taifa kwa njia ya kura kesho.


Tuliyoona yamechochea ari na dhamira yetu ya dhati ya kuomba ridhaa ya wananchi wa Tanzania na kushirikiana nao kuleta mabadiliko ya kweli.
Tulichokiona kimeniongezea ujasiri wa kuzidi kuuchukia umaskini

Tumejipanga vyema na kwa kutumia Ilani yetu, utayari wetu, uthubutu tulionao kuwaongoza Watanzania katika safari isiyo tu ya matumaini, bali ya mabadiliko, uhakika na ushindi

Ndugu zangu,

Mimi na nyinyi, tuna kila sababu ya kukubaliana na Mzee wetu, Kingunge Ngombale Mwiru, mmoja wa viongozi adhimu wa taifa hili ambaye amesema CCM imeishiwa pumzi, hivyo haina uwezo tena wa kutufikisha katika kilele cha mafanikio.

Mimi na ninyi Watanzania wenzangu tunapaswa kumuelewa kwa vitendo Baba wa Taifa, aliyesema chama kimoja kinachokaa kwa muda mrefu madarakani kinafikia hatua ya kujisahau. CCM ya leo iko mahututi.

Mimi na ninyi, tunapaswa kutambua kwamba maneno aliyopata kuyasema aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, marehemu Horace Kolimba kwamba 'CCM imepoteza dira' yana maana zaidi leo kuliko ilivyokuwa miaka 20 iliyopita.

Mimi na ninyi tunapaswa kujifunza kutoka kwa majirani zetu kama Kenya ambako wananchi walichukua hatua ya kuleta mabadiliko kwa njia za kidemokrasia mwaka 2002 na leo hii Wakenya hawamo tena miongoni mwa mataifa ya dunia ya tatu na maskini kama tulivyo sisi.





Mimi na ninyi, tunao wajibu wa kuikataa CCM kwa njia ya kura tukitumia kauli ya Mwenyekiti, Freeman Mbowe ambaye siku zote ametufundisha kwa kusema chama kile kile, chenye watu wale wale na ambacho kina sera, fikra na itikadi ile ile hakina uwezo wa kuongoza mabadiliko.

Ndugu zangu

Sina shaka hata kidogo kwamba, kwa njia ya sanduku la kura, Watanzania wameamua kuongoza mabadiliko ya maisha yao na ya taifa lao.


Ndugu zangu.

Rais Bora ambaye Tanzania inamhitaji wakati huu Watanzania wanapotaka mabadiliko ya kweli ni yule ambaye hata kabla hajakaa na wenzake na kuafikiana mambo ya msingi ya kisera, kiitikadi na kimaandeleo, yeye mwenyewe anayo maono ambayo anayaamini na kuyasimamia kwa dhati.

        Urais si kazi ya kubahatisha.
        Urais si jambo la pata potea.
        Urais ni wajibu na dhamana ya juu kabisa katika taifa
        Urais si mamlaka ya kutisha watu
        Urais ni wajibu wa kutoa dira ya taifa
       

Anayeomba urais anapaswa kuwa ni mtu aliyejiandaa na kuandaliwa vyema kifikra, kinidhamu, kimaadili kimikakati na kimaono

Ili uwe rais bora unapaswa kwanza kuwa mtumishi bora wa wananchi. Tunayo rekodi ya utumishi uliotukuka.

NDUGU zangu.

Ni jambo la kujionea haya sisi wenyewe kwamba miaka 54 baada ya Uhuru, Tanzania bado ni taifa masikini, tegemezi na linalozidi kudidimia.

Ni jambo baya zaidi kwamba, CCM kwa njia za hila na rushwa kinafanya juhudi kubwa kuzuia mabadiliko hayo.

Viongozi wakuu wa chama tawala, wanajaribu bila ya mafanikio kupandikiza mbegu mbaya vichwani mwa Watanzania ili wayakatae mabadiliko.

Watanzania tunalo chaguo moja tu, kukubali kubadilika.

Tunayo fursa ya kufanya kile kilichofanyika kwa mafanikio makubwa Zambia, Malawi, Kenya na kwingi kwingineko duniani.

Hatupaswi kusubiri hadi wananchi wakose subira na kupata hasira na kukosa uvumilivu wa kuingia mitaani na kuwang'oa watawala ving’ang’anizi wa aina ya CCM kama ilivyotokea, Libya, Tunisia, Irak na kwingineko.

Tunapaswa pia kujifunza kutoka nje ya Afrika ambako yako mataifa yaliyochupa kimaendeleo kwa sababu tu ya kupata uongozi madhubuti.

Siri wa mafanikio ya mataifa kama Malaysia, Korea Kusini, Thailand na Singapore ambayo miaka 50 tu iliyopita yalikuwa katika kiwango cha maendeleo kinachofanana na chetu ni UONGOZI wenye kuthubutu.


Ni fedheha kwetu kwamba, leo hii mataifa hayo ndiyo yamegeuka kuwa nchi wahisani, wafadhili na wawekezaji wakubwa.

Je, ni sahihi kuendelea kushangaa na kuyatamani maendeleo waliyopiga wenzetu hao? Jibu ni hapana.

Tunayo njia moja tu. Kuchukua hatua na kuleta mabadiliko yetu wenyewe.

Hatuwezi tukatoka hapa tulipo iwapo tutaendelea kuwakumbatia wale wale waliotukwamisha na ambao mawazo na mikakati yao ya kiuongozi ni ile ile iliyoshindwa kutukwamua kutoka hapa tulipo kwa zaidi ya miaka 54 sasa.

Tutakuwa tukijidanganya iwapo tutawaacha watu hao ambao kwa makusudi na kwa sababu zao walifikia hatua ya kukataa mawazo ya baadhi yetu ambayo yalikuwa yanaakisi maono, fikra na mikakati tofauti na ile ya kimazoea ambayo ndiyo hasa msingi wa kukwama kwetu.

Ndugu Watanzania wenzangu,
Naomba nimalizie kwa kusema yafuatayo ambayo nayasema tena leo kusisitiza kile ambacho nimekisema mara kadhaa:
1. Natambua kuwa uongozi ni dhamana. Mkinichagua kuwa Rais wenu, nitaienzi dhamana hiyo kwa utendaji uliotukuka na kwa uadilifu mkubwa.
2. Namuogopa Mungu, Nawaheshimu Watanzania. Naahidi kwamba nitawatumikia kwa uwezo, akili, uzoefu na nguvu zangu zote.
3. Watanzania wenzangu, mabadiliko yanaendana na kuthamini utu na kukataa hadaa ya hongo ili kuuza haki yako ya kuchagua.
4. Rushwa ya uchaguzi ndiyo sera ya CCM na ndiyo nyenzo yao ya kuwakandamiza Watanzania. Tukatae.
    Tuchague mabadiliko, tuichague CHADEMA. Tuchague wagombea wa UKAWA.
5.  Mabadiliko ni fikra. Ili tubadilike ni sharti tuanze sasa kufikiri na kutenda tofauti na ilivyo sasa.
6. Hatuwezi kuendelea kufikiri na kutenda kana kwamba hatuna dharura ya maendeleo. Tunaweza kujitegemea na kuleta maendeleo yetu wenyewe bila kutegemea wafadhili.
7.  Nchi nyingi zimefanikiwa kuondoa umaskini katika kizazi kimoja. Tujifunze kutoka kwao. Tanzania pia inaweza. Tuchague Mabadiliko.
8. Tunapaswa tangu sasa kuwa taifa linalotumia rasilimali zake kwa ufanisi zaidi kujiendeleza na siyo kwa kuwanufaisha wageni na kuwafanya Watanzania watwana katika nchi yao.
9.  Umaskini si joho la ufahari. Tuukatae. Lazima tuache kuwa taifa ombaomba. Hakuna faraja katika umaskini.
10.  Mabadiliko hayawezi kuletwa na CCM. Miaka zaidi ya hamsini ya utawala wake Watanzania bado ni maskini. Tusitegemee kuwa wanalo jipya hii leo.

Ndugu zangu. Ilani yetu imechambua na kuainisha masuala ya msingi ambayo serikali tutakayoiunda itayasimamia na kuyatekeleza hatua kwa hatua.

        •       Katiba
                – Hili ndiyo msingi wa umoja na mshikamano wetu ndani ya CHADEMA na ndani ya UKAWA.
                - Tutalifanya kwa umakini mkubwa huku tukiimarisha misingi ya umoja na mshikamano wetu kitaifa.

        •       Elimu
        •       Hiki ndicho kipaumbele chetu. Elimu Elimu Elimu
        •       Tunakwenda kuleta mapinduzi makubwa katika elimu.
        •       Mfumo mzima wa elimu yetu utafumuliwa
        •       Serikali nitakayounda itagharamia elimu bora tangu elimu ya msingi hadi Chuo Kikuu.

        •       Ajira
        •       Hili ni tatizo sugu
        •       Tusipotatua tatizo hili tunatayarisha bomu litakalolipuka
        •       Ni kwa kutambua umuhimu wa ajira ndiyo maana nawatambua na kuwaheshimu vijana wabunifu – bodaboda, mama ntilie na wamachinga.
        •       Hawa si wa kubezwa. Hawa si wa kuburuzwa na kutishwa. Wanapaswa kuimarishwa ili waimarike kibiashara na kiuchumi
        •       Hawa kwangu ni mashujaa wa ajira. 


        •       Afya

        •       Huku kunatakiwa mapinduzi makubwa.
        •       Tumejizatiti kujenga Hospitali za Rufaa zenye hadhi katika kila wilaya
        •       Afya ndiyo msingi wa mafanikio yote mengine. Pasipo afya hakuna tija
        •      
        •       Miundombinu

        •       Hii ndiyo injini ya uchumi wa mataifa yote yaliyoendelea
        •       Miundombinu ni zaidi ya barabaraba
        •       Miundombinu ni reli, bandari, viwanja vya ndege na kadhalika.
        •       Tumejipanga vyema kuimarisha eneo hili kwa kujenga reli mpya




        •       Maji
        •       Hili ni tatizo mama
        •       Tunazidiwa hata na mataifa yaliyo jangwani. Hii ni aibu kubwa
        •       Tunakwenda kujenga upya miundombinu ya maji.
        •       Tatizo la uhaba wa maji litakuwa historia

        •       Michezo, Sanaa na Utamaduni
        •       Tumekuwa wasindikizaji katika eneo hilo zima
        •       Tunayo mikakati ya kulikwamua taifa kutoka huko
        •       Tanzania haitakuwa tena kichwa cha mwendawazimu katika ulimwengu wa michezo

Tunayo Ilani ya CHADEMA na UKAWA inayotoa DIRA YA MABADILIKO katika sekta na maeneo yote hayo.

Ndugu zangu Watanzania. Mkituamini, mkatuchagua. Hatutawaangusha.
USHINDI WETU NI USHINDI WA WATANZANIA
NI WAKATI WA MABADILIKO
TUNAOMBENI KURA
Ahsanteni kwa kunisikiliza





PIUS MSEKWA  - MWALIMU NYERERE NA MSIMAMO WA DEMOKRASIA KATIKA UCHAGUZI











Mwalimu Nyerere alikuwa na uwezo wa kuona
Mwalimu Nyerere alikuwa na uwezo wa kuona mbali, hata alipopingwa baadaye waliompinga walikiri ukweli wa maono yake-PIUS MSEKWA
By Pius Msekwa
Ni dhahiri kwamba Mwalimu Nyerere anakumbukwa kwa mambo mengi ya msingi aliyoyapa kipaumbele wakati wa uongozi wake.  Jambo mojawapo alilisema Julai 29 Julai, 1985, kwamba: “Kazi iliyokuwa muhimu kuliko zote kwangu mimi, ilikuwa ni kujenga Taifa lenye umoja kwa msingi wa heshima na usawa wa binadamu”.
Lakini yapo mambo mengine mengi ya uongozi wake ambayo tunapaswa kuyakumbuka na kuyaenzi , hususan suala la uadilifu katika uongozi (au maadili ya uongozi), Azimio la Arusha, miiko ya uongozi,  mapambano yake dhidi  ya rushwa,  ufisadi na mengineyo.
Pamoja na hayo  kuwa maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, nimeona ni vyema nitoe mchango wangu kwa kukumbusha juu ya msimamo wake thabiti juu ya umuhimu wa demokrasia katika uchaguzi wa viongozi wetu.
Wosia wake kuhusu makosa yanayopaswa kuepukwa  wakati wa uchaguzi:
Katika kitabu chake alichokiandika mwaka 1962 kinachoitwa “Tujisahihishe”,  Mwalimu Nyerere aliorodhesha makosa ambayo alisema yanatokana na ubinafsi na akawaasa Watanzania wajiepushe na makosa hayo.
Alisema: “Kosa jingine linalotokana na ubinafsi tunalifanya wakati wa kuchagua viongozi. Wakati mwingine hufanywa na wanachama, wakati mwingine hufanywa na viongozi wenyewe. Viongozi wetu hawana budi watokane na watu, bila hila, vitisho, rushwa, au ujanja wa aina yoyote. Lakini mara nyingi wanachama huchagua viongozi bila kufikiri kwa makini kama viongozi hao wanaiweza, au hawaiwezi, ile kazi wanayochaguliwa kuifanya…’’
Mwalimu Nyerere alivyopigania demokrasia katika uchaguzi:
Enzi za ukoloni, utawala wa kikoloni ulipanga kwamba uchaguzi mkuu wa kwanza wa wajumbe wa baraza la kutunga sheria ufanyike  Septemba mwaka 1958. Katika kufanya maandalizi ya uchaguzi huo, utawala huo ulitunga sheria mahsusi, ambayo ilikiuka kabisa misingi ya demokrasia katika uchaguzi, kwa lengo eti la kujihakikishia kwamba Wazungu na Wahindi wanaingia katika baraza hilo kwa idadi iliyo sawa na Waafirika (ambao walikuwa ni wengi zaidi).
Sheria hiyo lijulikana kama “sheria ya kura tatu”, ambapo kila mpiga kura aliwekewa sharti kwamba ili kura yake iweze kuwa halali, lazima apige kura tatu kwa pamoja, yaani kura moja kwa mgombea Mzungu, kura ya pili kwa mgombea Mhindi au Singasinga na kura ya tatu kwa mgombea Mwafrika.
Demokrasia katika uchaguzi inataka kila mpiga kura awe na kura moja tu, ambayo atampigia mgombea yeyote yule atakayemuona yeye kuwa anafaa.
Kwa hiyo hili suala lakulazimisha kura tatu lilikuwa linakiuka msingi huo wa demokrasia. Kwa sababu hiyo, wanachama na  viongozi wengi wa TANU, waliipinga sheria hiyo kwa nguvu, na wakapanga kususia uchaguzi wenyewe, wakidhani kuwa njia hiyo ingeweza kuulazimisha utawala wa kikoloni kusikiliza madai yao ya kutaka sheria hiyo ifutwe.
Kumbe Mwalimu Nyerere alikuwa ‘kiona mbali’ zaidi kuliko wenzake wengi. Alitambua kuwa kususia uchaguzi kutawanyima Waafirika fursa ya kuingia kwenye Baraza la Kutunga Sheria na kwamba Wakoloni watatumia mwanya huo kupitisha sheria nyingine za kuchelewesha uhuru wa Tanganyika, kwa kisingizio kwamba kitendo chao cha kususia uchaguzi kinadhihirisha kwamba Waafrika hawajawa tayari kujitawala wenyewe.
Ndipo wajumbe walipokwenda kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa TANU uliofanyika Tabora mwezi Januari 1958, wakiwa wamejiandaa kupitisha azimio kali la kususia uchaguzi huo wa kura tatu.  Kwa upande wake, Mwalimu Nyerere naye alienda kwenye mkutano huo akiwa amejiandaa kujaribu kuwashawishi wajumbe wenzake wakubali kushiriki katika uchaguzi huo. Katika hali hiyo, kwa hakika alikuwa na kazi ngumu  mbele yake.
Lakini kwa kutumia vipaji vyake vya uwezo mkubwa wa kushawishi alivyokuwa amejaliwa na Mwenyezi Mungu, alifanikiwa kufanya hivyo;  na mkutano huo ukatoka na azimio  la kushiriki kwenye uchaguzi huo.
Lakini ilikuwa kazi ngumu, kwani  aliyekuwa Katibu Mkuu wa TANU, Zuberi Mtemvu, hakuridhika na uamuzi huo, akajitoa kwenye TANU na kuunda chama chake kipya cha African National Congress (ANC).
Hata hivyo, matokeo ya uchaguzi huo yalithibisha busara za Mwalimu Nyerere, kwani kutokana  na mkakati ambao Mwalimu Nyerere aliubuni wa kusimamisha wagombea Wazungu na Wahindi ambao walikuwa  wakiunga mkono juhudi za TANU za kudai uhuru, Chama cha TANU kilifanikiwa kushinda katika majimbo yote 10 yaliyokuwapo ya uchaguzi, na wagombea wake walipita bila kupingwa katika majimbo mengi.
Mfano mwingine wa kupigania uchaguzi wa kidemokrasia
  Uchaguzi huo wa kwanza ulifuatiwa na uchaguzi wa pili, ambao ulipangwa kufanyika Septemba mwaka 1960.  Katika uchaguzi huo wa pili, sheria ya kura tatu ilikwisha kufutwa, na idadi ya majimbo iliongezwa hadi kufikia 71.
Matokeo ya uchaguzi huo wa pili yalikuwa ni kwamba wagombea wa TANU walipita bila kupingwa katika majimbo 58 miongoni mwa hayo 71, na katika yale majimbo mengine 13 ambayo yalikuwa na ushindani, wagombea wa TANU walishinda katika majimbo yote, (mmoja wao akiwa ni mwananchama wa TANU aliyekuwa amejisimamisha kama mgombea binafsi).
Wagombea wanapopita bila kupingwa, maana yake ni kwamba hakuna uchaguzi unaofanyika katika majimbo husika. Maana yake nyingine ni kwamba wapiga kura wa majimbo hayo wananyimwa haki yao ya msingi ya kupiga kura. Ni dhahiri kwamba hali hii ya kunyima watu fursa ya kupiga kura, inadidimiza demokrasia katika uchaguzi.
Mwalimu Nyerere alitambua hivyo, na alitambua vile vile kwamba hali hiyo inasababishwa na vyama  vingine kutosimamisha wagombea wao, wakiogopa kupoteza muda wao huku wakijua kwamba kutokana na nguvu ya upendo kwaTANU ilivyokuwa kubwa , walijua kwamba hapakuwa na uwezekano wa kuwashinda wagombea wake.
 Kwa hiyo, ili kurejesha demokrasia ya ushindani katika uchaguzi, Mwalimu Nyerere alianza mchakato wa kutunga Katiba mpya ya mfumo wa chama kimoja cha siasa, ambayo ingewezesha wanachama wake kushindanishwa katika uchaguzi, na kwa hiyo kuwapatia wapiga kura fursa ya kutumia haki yao ya msingi ya kuwachagua viongozi wao.
Pius Msekwa ni kada mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika chama, Bunge na Serikali


MJUE GHALIB S MOHAMED WA HOME SHOPING CENTRE, MHUJUMU UCHUMI MKUU TANZANIA NA MPANGO WA WIZI WA KURA


Anaitwa Ghalib S Mohamed ni Mwenyekiti wa kampuni ya Alosco inayomiliki makampuni mengine zaidi ya kumi ikiwemo Supermarket za Home Shopping Centre



Ghalib S Mohamed, fisadi na jangili ambae tangu rais Jakaya Kikwete aliposhika hatamu mwaka 2005, alipewa fursa za kufanya biashara bila kulipia ushuru bidhaa alizokuwa akiingiza nchini kwa ubia na familia ya Rais Jakaya Kikwete. Leo hii kupitia mianya hii ya kifisadi na unyonyaji wa jasho la watanzania, Ghalib ni moja kati ya matajiri wa kubwa Tanzania anae miliki Mali nyingi za kifahari, Majengo, Magari na biashara nyingi za nyuma ya pazia.

Ghalib ana miliki jumba lenye gharama ya bilioni 13 za kitanzania iliyo jengwa kwenye eneo la heka 11 huko Kinyerezi. Eneo hilo ambalo lilimefanya familia zaidi 33 kuhamishwa bila kibali maalum kwa ajili ya ujenzi wa jumba moja la mtu mmoja. Ghalib huyu huyu ana miliki nyumba 4 Masaki na sasa ana malizia jumba lingine la kifahari mtaa wa Lincoln Masaki ambalo lina jengwa na wakandarasi kutoka china. Ghalib ana miliki magari  tofauti ya kifahari ikiwemo Rolls Royce, Bentley, Ferrari magari kadhaa aina ya Range Rover yenye thamani zaidi ya billioni 3 za kitanzania.






Kazi kubwa ya kifisadi ni ile ya usafirishaji bidhaa bila kulipa ushuru kupitia kampuni yake ya usafirishaji ya Silent Ocean inayosimamiwa na mdogo wake anayeitwa Salaah ambayo makao makuu yake yapo China. Salaah ambae kwa sasa amefanywa balozi mdogo wa Tanzania nchini China bila kuzingatia historia yake ya uhalifu wa kutumia silaha na kutishia kuuwa watu kwenye kumbi tofauti za starehe, zaidi ya hapo salaah hana elimu wala historia ya kidiplomasia lakini uswahiba wa familia yao na JK umempa nafasi hii kubwa kabisa katika Taifa letu.

WIZI WAKE KWA SERIKALI NA TAIFA

hivi karibuni Ghalib na washirika wenzie (familia ya Kikwete) wameanza utaratibu wa kuhamisha makazi yao nchini Tanzania na kwenda kuishi nchi za ukanda arabu
tayari kuanza mkakati huo wamekuja na mpango huu wa kulibia taifa na serikali kwa dakika za mwisho



Ajab ni kwamba Leo hii Ghalib ndio nguzo kuu ya ufadhili wa CCM na familia za viongozi wa CCM. Kwa Lugha nyepesi, ghalib ndio anafanya mipango yote na mikakati ya CCM na Serikali iliyopo madarakani.  Mkakati mkubwa alionao sasa ni huu wa kuaratibu wizi wa kura ambao Ghalib na maswahiba wake wamemwaga pesa nyingi sana ili kufanikisha wizi mkubwa wa kura katika historia ya Taifa hili wakijua dhahiri Magufuli hana asilimia 30 ya kura za Watanzania.


MPANGO WA WIZI WA KURA UCHAGUZI WA MWAKA HUU.

Baada ya kutafuna rasilimali za watanzania kwa ufisadi uliotukuka chini ya mbawa za Rais kikwete na familia yake sasa ndio ataongoza kamati ya ufundi ya wizi wa kura kuanzia tar 24 oktoba.

Ghalib akiwa pamoja na Faroukh Bagonza wa kampuni za mafuta ya TSN na Supermarket za TSN wame ratibu wizi wa kura kwa kuagiza masanduku yaliyo jaa makaratasi ya kupigia kura kutoka Msumbiji na vifaa vingine haramu vya kupigia kura ambavyo vimehifadhiwa kwenye Godauni (maghala) ya Faroukh Mtaa wa Gerezani, Mnazi moja. 

Ghalib na Faroukh wakishirikiana na jangili mwenzao Abdulrahman Kinana wiki iliyopita wamenunua magari manne kutoka kampuni ya Toyota Tanzania Ltd iliyopo barabara ya Pugu. Magari hayo yatatumika kusafirisha makaratasi ya kura batili na kutumika kama magari feki ya wasimamizi wa kimataifa wa SADC.  Mpango ni kupeleka gari mbili Zanzibar na mbili zitakuwa Tanzania Bara. Gari hizo aina ya Toyota Landcruiser Hardtop (2) zenye namba za usajili T 471 DFC na T 469 DFC zenye chasis namba TEEB71 – 90 - 7026583 na TEEB71 – 00 – 7026617. Pia wamenunua Toyota Hilux Double Cabin (2) zenye namba za usajili T 468 DFC na T 470 DFC zenye chasis namba AHTFR22G10 – 6105538 na AHTDR22G00 – 6105546.


 mmoja wa wana familia akiwa ikulu na Rais Kikwete
MTOTO WA GHARIB S MOHAMEDY AKIWA NA RAIS JK KIKWETE


GHARIB S KIKWETE ,NDUGUYE WAKIWA SAMBAMBA NA MAREHEMU ABDALAH KIGODA (WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA) 

KULIPA MISHAHARA YA SERIKALI
MR.GHARIB ndiye aliyehusika moja kwa moja kulipa mishahara ya viongozi wa serikali (wabunge na mawaziri ) na kuendesha bajeti yao yote kwa kipindi chote walichokua wakifanya biashara ya magendo kwa idhini ya serikali ya Mh Jk Kikwete.







Post a Comment: