Friday, 8 December 2017



Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Elisha Mghwira ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Mghwira ametangaza uamuzi huo alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) unaofanyika mkoani Dodoma.
RC huyo wa Kilimanjaro amesema amefikia uamuzi huo kutokana na utendaji wa serikali ya awamu ya tano, hivyo ameona ni vyema ajiunge na CCM ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Nimeiona CCM inayobadilika, nimeona juhudi za kila mtu, ninaiona CCM inayoanza kukataa rushwa, nimeiona CCM inayoanza kulipeleka taifa mbele, amesema Mghwira kwenye mkutano huo na kuongeza.
Ninataka niseme kwamba baada ya kufanya kazi chini ya serikali hii kwa miezi takribani sita saba sasa ninaona nina sababu ya kutangaza kwamba ninapenda kuungana na Chama cha Mapinduzi.”

Post a Comment: