Friday 8 December 2017


Tundu Lissu akiendela na matibabu.
JESHI la Polisi limekwama kumhoji Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), akiwa hospitalini Nairobi, Kenya baada ya kiongozi huyo kusema kwamba polisi wa Tanzania hawawezi kumhoji akiwa nchini Kenya au kwingineko nje ya mipaka ya nchi.
 
Kauli ya Lissu imekuja siku 10 tangu Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro, kuiambia Nipashe kuwa wametuma askari wawili kwenda Nairobi kuchukua maelezo ya Lissu, baada ya Mbunge huyo kukubali kuhojiwa.
 
“Hadi sasa Mwanasheria Mkuu wa Tanzania hajamwomba Mwanasheria Mkuu mwenzake wa Kenya ruhusa ya mimi kuhojiwa na Polisi wa Kenya juu ya shambulio hilo kama inavyotakiwa na sheria husika za nchi yetu,” amefafanua Lissu ambaye ni mwanasheria kwa taaluma.

Post a Comment: