Mbunge Nassari avamiwa na Watu Wasiojulikana
MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari usiku
wa kuamkia leo yeye na familia yake walivamiwa nyumbani kwao na kundi
la wahalifu wasiojulikana wakiwa na silaha na kufyatua risasi kama
mvua kwa lengo la kumshambulia Mbunge huyo.
Hata hivyo kelele za mbwa na kutojua nyumba anayolala Nassari kati ya
nyumba tatu zilizopo eneo hilo zimesaidia kumwokoa ambapo watu hao
walifanikiwa kumuua mbwa wake mkubwa huku Mbunge huyo na mkewe
wakifanikiwa kutoroka na kutokomea kizani usiku na baadaye kutoa taarifa
Polisi.
Kabla ya tukio hilo, Mbunge Nasari mchana wa Ijumaa alitembelea
wahanga wa tukio la kushambuliwa kwa mapanga kwa baadhi ya wananchi
katika kata ya Makiba siku moja kabla ya marudio ya uchaguzi mdogo wa
udiwani.
Post a Comment: