Friday, 8 December 2017


WABUNGE wa CHADEMA, Peter Lijualikali na Suzan Kiwanga pamoja na washtakiwa wengine 36 ,leo Ijumaa, Desemba 8, 2017 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kusikiliza maombi ya kupatiwa dhamana kwenye kesi inayowakabiri.
Mahakama imesema itatoa uamuzi saa 9 alasiri leo baada ya mabishano ya kisheria juu ya dhamana za Wabunge wa CHADEMA, Peter Lijualikali na Suzan Kiwanga na washtakiwa wengine 36.
Itakuwambukwa kuwa, Washtakiwa hao kwa ujumla hao wanakabiliwa na mashtaka kadhaa likiwemo la kuchoma moto ofisi za serikali katika uchaguzi wa mdogo wa madiwani uliomalizika hivi karibuni mkoani Morogoro.

Post a Comment: