Wednesday 29 November 2017

Viongozi wa CUF ya Lipumba Hapatoshi Waanza Kushikana Uchawi


Viongozi wa (CUF) chini ya Katibu Mkuu na Lipumba wameanza kutupiana lawama na kushikana uchawi, Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF Mbarala Maharagande amefunguka na kusema Maalim Seif analindwa na haki na si ushirikina.

Mbarala Maharagande amedai kuwa Lipumba na kundi lake ni watu ambao wanaamini sana ushirikina na kutegemea ushirikina kufanikisha mpamgo wao kuivuruga na kuisambaratisha Taasisi ya CUF.
 
"Lipumba na wafuasi wake ni watu wanaoamini sana mambo ya ushirikina katika kufanikiwa mipango yao michafu dhidi ya Taasisi ya CUF. Mara kadhaa wameonekana kutumwa wafuasi wake kwenda kununua Mbuzi kwa ajili ya kazi hiyo katika mnada wa Vingunguti. Kamati ya ushirikina inaongozwa na Abdul Kambaya na Hamisi Hassan kwa upande wa Tanzania Bara na Mohamed Thiney na Nassor Seif kwa upande wa Zanzibar" aliandika Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF Mbarala Maharagande
 
Mbali na hilo Mbarala amesema kuwa Profesa Lipumba na kundi lake wameshindwa kuigawa CUF kama ambavyo walikuwa wakitegemea na kudai uchaguzi mdogo wa udiwani umeweza kutoa majibu kwani wagombea wote wa Lipumba wamepata kura chache sana na kuonekana wazi kuwa watu hao hawakubaliki katika jamii.
 
"Lipumba na wafuasi wake wameshindwa kuigawa CUF na mbeleko ya CCM inakaribia kukatika kutokana na kutoona faida yao hasa katika ushindani wakati wa uchaguzi. Watazania washawafahamu kuwa ni vibaraka, wasaliti na wachumia tumbo, hawapo kwa dhati ya kutaka Mabadiliko ya kweli kisiasa kutokea hapa nchini. Mgombea wa Lipumba katika Kata ya Reli, Mtwara Mikindani kushika nafasi ya nne kwa kupata kura 21 baada ya CCM, CHADEMA, na ACT katika Jimbo linaloongozwa na Mbunge kutoka ‘CUF MAKINIKIA’ ni salamu tosha kwa Maftaha Nachuma na Lipumba kuwa hawakubaliki na hawana mchango wa maana kwa CCM" alisisitiza Mbarala
 
Pia Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF Mbarala Maharagande amekanusha taarifa inayosema kuwa Maalim Seif anashirikiana na waganga wa kienyeji na kuwa mambo yamezidi kuwa magumu kwake.
 
"Eti Maalim Seif anashirikiana na Waganga na mambo yanazidi kuwa magumu kwake! Mambo yepi magumu na Spika anatakiwa atangaze rasmi lini Wabunge halali wa CUF waanze utumishi wao Bungeni kutokana na maamuzi ya Mahakama. Msemaji wa Lipumba, David Maphone kahamia kuwapigia kampeni wagombea wa UVCCM sasa"

Post a Comment: