Thursday 30 November 2017

Dr. Heshima


Bunge Lawatosa Wabunge 8 wa CUF Ambao Waliovuliwa Uanachama


Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetoa ufafanuzi juu ya maamuzi ya mahakama kuhusu wabunge 8 wa CUF ambao walivuliwa uanachama na kupoteza sifa kuwa wabunge na kusema katika maamuzi ya mahakama hakuna sehemu imesema watu hao wapewe Ubunge.

Katibu wa Bunge amesema kuwa amekuwa wakiona kwenye mitandao ya kijamii na katika vyombo vya habari taarifa mbalimbali zikisema kuwa wabunge hao ambao walivuliwa uanachama na CUF kuwa wanatakiwa kurudishiwa ubunge wao na kudai hakuna jambo la namna hiyo kwa kuwa nafasi zao tayari zilijazwa na Tume ya Uchaguzi. 

Post a Comment: