Sio kila anayepata ujauzito amependa, Rais alitazame upya” – Ester Matiko
June 22, 2017 President Magufuli
alikamata Headlines baada ya kutoa tamko akiwa ziarani Pwani kuwa
katika Serikali ya Awamu ya Tano hakutakuwa na mwanafunzi aliyepata
ujauzito akiwa shule kuendelea na masomo baada ya kujifungua.
Tamko hilo liliibua hisa tofauti kwa wadau mbalimbali hasa watetezi
wa haki za wanawake na watoto wa kike wakisema inawanyima watoto wa kike
haki ya kupata elimu kwa sababu wengi wanaopata ujauzito wakiwa shuleni
hawakusudii bali wengine hubakwa.
Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko
ambaye ni mmoja wa wadau wanaofanya jitihada kumlinda mtoto wa kike na
kuhakikisha anapata elimu na amekuwa na hisia tofauti na tamko la Rais
JMP.Akihojiwa na Ayo tv mheshimiwa mbunge amesema
”Inawezekana Rais
Magufuli anatamka kabla hajashauriana na watendaji wake kupata picha
halisi ya kinachoendelea Tanzania na madhara ya watoto wa kike.
“Mtoto anaweza kupata ujauzito kutokana na umbali ambapo
hukutana na vishawishi; anaweza kubakwa na kushawishiwa kwa sababu ya
umbali anaotembea…namuomba Rais Magufuli afikirie tena. Unaweza
kukitamka kitu baadaye ukakitafakari ukapata mawazo ya aina mbalimbali.”
– Ester Matiko.
Post a Comment: