ZIARA YA KAMATI YA BUNGE YA BAJETI DAR ES SALAAM KATIKA TAASISI ZA MUHIMBILI, DART NA IFM
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doroth Mwanyika akijibu hoja
mbalimbali za Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakati wajumbe hao
walipotembelea Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM). Katikati ni Mwenyekiti
wa Baraza la Chuo hicho, Prof. Lettice Rutashobya na Mwenyekiti wa
Kamati ya Bajeti, Mhe. Hawa Ghasia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi akiwaeleza masuala mbalimbali kuhusiana na huduma ambazo hospitali hiyo inazitoa kwa Kamati ya Bunge ya Bajeti ambayo pamoja na mambo mengine ilitembelea hospitalini hapo kujionea shughuli zinazofanywa ikiwemo upasauaji wa moyo kwa wagonjwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Hawa Ghasia akielekezwa jinsi ya kutumia risiti ya Mwendokasi kwa ajili ya kuingia kituoni kusubiri basi.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiwa ndani ya Basi la Mwendo Kasi wakielekea Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam, wajumbe hao walikuwa wakikagua mfumo wa kukusanya fedha za nauli kwa mabasi hayo uliotengenezwa na Kampuni ya Maxcom.
Post a Comment: