Waziri Ummy afanya ziara kituo cha afya Matei, Kalambo
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka watoa huduma za afya
katika kituo cha afya cha Matei wilayani Kalambo kutoa huduma bora kwa
wanawake wajawazito
Rai hiyo imetolewa jana na Waziri huyo
alipokuwa kwenye ziara ya kikazi wilayani hapo na kutembelea hospitali
hiyo pamoja na kuongea na watumishi wa sekta ya afya kujua changamoto
zinazowakabili
Alisema wajawazito wanapaswa kupata
huduma bora kila wanapofika kliniki kila mwezi kwa kuangaliwa mfano
dalili za kifafa cha mimba ,wigi wa proteini pamoja na viatarishi
vingine vinavyoweza kusababisha uzazi pingamizi na hivyo kupelekea
vifo kwa mama au mtoto wakatiwa kujifungua
“Nawapongeza sana kwa kutenga
dirisha la wazee ila kusiwepo tu dirisha bali muwape dawa wazee wasio
kuwa na uwezo,hivyo kama kuwakatia mfuko wa bima ya jamii (CHF)ni
gharama basi wapatieni vitambulisho vya matibabu bure ili wazee wakija
kwenye matibabu wasije na barua za watendaji wa vijiji,” alisema Ummy.
Kwa upande wa madawa Waziri Ummy
amewaambia watendaji hao hakuna masharti magumu ya ununuzi wa madawa na
vifaa tiba kwa kutumia pesa za CHF“nimeshawaambia MSD ndani ya masaa
ishirini na nne umeagiza vitu MSD hana,ndani ya masaa hayo kama hana
unaruhusiwa kwenda kununua unapotaka kwenda”hivyo ni vyema wakapitisha
wadhaburi watakaokuwa wananunua.
“Tangu serikali hii iingie
madarakani imefanya mabadiliko makubwa katika upatikanaji wa dawa kwa
kuongezwa bajeti ya dawa kwa asilimia kubwa hizi changamoto ndogondogo
zipo ila mwisho wa siku wananchi wanahitaji dawa,hivyo kuhakikisha dawa
zile muhimu zinapatikana wakati wote.” alisema Ummy.
Hata hivyo amewataka kuwapa kipaumbele
wale wanaotumia bima ya afya,nataka kuona mnaongeza wananchi
watakaotumia bima ya afya kwenye matibabu ili kuweza kutatua changamoto
za sekta ya afya Upande wa Malaria Waziri Ummy vipimo vya haraka vya malaria vya MRTD ni bure pamoja na dawa ya kutibu Malaria’ALU’ ni bure ”asije kuwaambia mtu kipimo hicho utoe pesa,sindano kama mtu amezidiwa na maralia kali ni bure,” alisisitiza Waziri Ummy.
Akiongelea ugonjwa wa Kifua Kikuu”TB”
Waziri huyo alisema ni wakati wa kuwaambiwa watu Tb inatibika kwani
katika kila watu mia moja wanaoumwa kifua kikuu na kutumia dawa watu
tisini wanapona kabisa na wanaendelea na shughuli zao.
Post a Comment: