WAZIRI MKUU AWAONYA WEZI WA DAWA HOSPITALI .
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Sikonge Mjini jana Agosti.10.2017 katika viwanja vya Tasaf Waziri Mkuu yupo Mkoani
Tabora kwa ziara ya Kikazi
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewaonya
wamiliki wa maduka ya madawa ya binadamu na watumishi wa sekta ya afya
wanaochukua dawa ambazo zinapaswa kupelekwa katika Hospitali za Serikali
ili kuwahudumia wananchi na kuziweka katika maduka yao.
Mhe. Majaliwa alitoa kauli hiyo jana Wilayani Sikonge katika mkutano wa hadhara na wananchi katika Kiwanja cha TASAF.
Alisema
kuwa vitendo hivyo ndivyo vimekuwa vikisababisha upungufu wa dawa
katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali mbalimbali za Serikali na
kufanya baadhi ya wananchi kuendelea kuteseka na maradhi kwa sababu ya
kushindwa gharama za ununuzi wa dawa katika maduka ya watu binafsi.
Waziri
Mkuu Mhe. Majaliwa aliwaonya watumishi wa afya na wamiliki hao wenye
tabia hizo kuacha mara moja endapo watabainika kuendesha vitendo hivyo
watachukuliwa hatua kali.
Alisema
kuwa Serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili kununua dawa ili
zinasaidia kutoa huduma ya matibabu kwa wananchi wake lakini kuna baadhi
ya watumishi wa afya wasio waadirifu ambapo wamekuwa wakitorosha dawa
na kuwauzia wamiliki wa maduka ya dawa na ksuababisha upungufu katika
vituo vya Serikali.
Waziri
Mkuu kuwa Serikali haiwezi kuwavilimia watumishi wa afya wasio
waaminifu wanaochukua dawa na kuzipeleka katika maduka binafsi huku
wakisababisha upungufu katika baadhi ya hospitali za umma.
Alisema kuwa hospitali ni lazima ziwe na dawa za kutosha ili kuepusha usumbufu kwa wananchi.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu ameikabidhi Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa
wa Tabora orodha ya watu wenye tabia ya kuwarubuni wakulima wa tumbaku
na kununua katika mfumo ambao si rasmi na kisheria (soko huria) na
kuwanyonya ili wahojiwe.
Alisema
kuwa watu hao kwa muda mrefu ndio wamekuwa wakiwanyonya wakulima
kununua tumbaku zao kwa vishanda na kuwa fedha ambazo zinazidi
kuwakandamiza.
“Nina
majina ya watu ambao wamekuwa wakipita kwa wakulima na kununua tumbakuza
wakulima kwa njia ya vishada ….huku wakiwanyonya kwa kuwapa fedha
kidogo nawataka waache mara moja.” Alisisitiza Mhe. Waziri Mkuu.
Aliongeza
“leo siwataji majina yao lakini nakuachia Mkuu wa Mkoa ili wewe na
Kamati yako ya Ulinzi na Usalama muwaite na kuwahoji na kisha ziwaonye
wasiendelee na biashara hiyo, kama wanataka kuendelea na uuzaji wa
tumbaku wahakikishe wanayopeleka sokoni ni ile waliolima wenyewe na sio
ya kununua kwa wakulima”
Aidha
Waziri Mkuu alitoa onyo kwa watumishi wa umma ambao wamekuwa na tabia ya
kugonja wakulima walime tumbaku na wakisha kuvuna na kukausha wao
wanakwenda kununua kwa ajili ya kuipeleka katika makampuni ya tumbaku.
Alisema mtumishi hakatazwi kulima kulima tumbaku bali atakiwi kununua tumbaku kutoka kwa mkulima.
Waziri
Mkuu huyo aliwaagiza viongozi wa Mkoa wa Tabora kukamata watu wote
wanajihusisha na ulanguzi wa tumbaku ya wakulima na kuongeza kuwa
watakamatwa wakiwa na tumbaku ya ulanguzi ichukuliwe pamoja na chombo
cha usafiri kinachotumika kusafirishia.
Alisema kuwa tumbaku yote inauzwa kupitia vyama vya msingi na kila mtu atauza tumbaku kwa kiwango alicholima.
Post a Comment: