WAZIRI MKUU APOKEA MSAADA WA MAGARI KUTOKA KAMPUNI YA FOTON
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akipokea Funguo za Magari matatu yenye thamani ya
Dola za kimarekani 99,700 ambayo amekabidhiwa na Naibu Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Foton International kutoka China Bwana Zhao Xiano
Kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo nchini Tanzania,
wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Meneja masoko wa kampuni ya Simba
Motors Taanzania Bibi Ifigenia Salazar na kutoka kulia ni Afisa masoko
wa Foton International, Bwana Fan Liang. Makabidhiano hayo yamefanyika
leo ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es salaam. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia moja ya magari aliyokabidhiwa na Naibu
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Foton International kutoka China Bwana
Zhao Xiano Kwa ajili ya kusaidia shughuli zamaendeleo nchini Tanzania Makabidhiano hayo yamefanyika leo ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es salaam.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa magari matatu yenye thamani ya Dola za Marekani 99,700 kutoka Kampuni ya Foton International Trade Co. Ltd ya nchini China.
Amepokea
msaada huo leo (Jumatano, Agosti 9, 2017) jijini Dar es Salaam, ambapo
amesema magari hayo yatatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo
ya jamii nchini. Magari hayo ni Sauvana SUV moja na Tunland Double cabin
mbili.
“Nashukuru
kwa msaada huu wa magari uliotolewa na Kampuni ya Foton kwa Serikali
yetu. Magari haya yanaweza kutumika katika Hospitali za wilaya kwa ajili
ya usambazaji wa dawa na vifaa tiba pamoja na kutolea elimu mbalimbali
kwa umma.”
Pia,
Waziri Mkuu ameikaribisha Kampuni hiyo kuja nchini kuwekeza katika
ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha magari. Amesema mbali na utulivu wa
kisiasa uliopo Tanzania, pia kuna sera na mazingira mazuri ya uwekezaji.
Kwa
upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Zhao Xiao
amesema wametoa msaada huo wa magari kwa ajili ya kusaidia shughuli za
maendeleo zinazofanywa na Serikali ya Tanzania hususan maeneo ya
vijijini.
Bw.
Xiao amesema Kampuni ya Foton inatengeneza magari 700,000 kwa mwaka,
ambayo yanauzwa katika nchi 125 duniani. Amesea ifikapo mwaka 2020
wanatarajia kuongeza uzalishaji na kufikia magari milioni 1.4 kwa mwaka.
Kuhusu
suala la kuja kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha magari
nchini, Bw. Xiao amesema wanampango wa kuwekeza nchini kwa kuwa kuna
fursa nzuri za uwekezaji na uhakika wa masoko katika nchi zingine za
Afrika Mashariki.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, AGOSTI 9, 2017
Post a Comment: