WAKENYA KUSUKA AMA KUNYOA LEO
Leo Agosti 8, 2017, takribani
Wakenya milioni 19 wanatarajia kupiga kura kuwachagua rais, magavana wa
kaunti, wabunge, maseneta, wawakilishi wa wanawake na wawakilishi wa
kata.
Vituo karibu vyote vya kupigia kura
vimefunguliwa rasmi tangu saa 12: 00 alfajiri, huku wapiga kura
wakijitokeza vituoni kuanzia majira ya saa 9 usiku tayari kupanga foleni
kwa ajili ya uchaguzi huo.
Kwa mara nyingine, Uhuru Kenyatta wa Chama cha Jubilee na Raila Odinga
wa Muungano wa Upinzani (NASA), wanaonekana kuwa na ushindani mkubwa
katika kinyang’anyiro hicho. Kenyatta ni mtoto wa Rais wa kwanza wa
Kenya, Mzee Jomo Kenyatta na Odinga ni mtoto wa makamu wa rais wa kwanza
Jaramogi Oginga Odinga.
WAKATI HUO HUO
Waziri awahakikishia Wakenya usalama wakipiga kura
Kumekuwa na wasiwasi kuhusu hali ya usalama nchini Kenya, hasa kutokana na ushindani mkali unaoshuhudiwa kati ya wagombea urais wawili wakuu huku wananchi wao wakiwa bado wanakumbuka ghasia zilizozuka baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Aidha, hivi karibuni Meneja wa TEHAMA wa Tume ya Uchaguzi IEBC, Chris Musando aliuawa na watu wasiojulikana. Wakati huo Kaimu Waziri wa Usalama, Dkt. Fred Matiang’i amewahakikishia Wakenya kwamba usalama umeimarishwa.
Wananchi wakiwa kwenye vituo vya uchaguzi mapema alfajiri leo.
Maofisa wa Tume ya Uchaguzi wakiandaa fomu kwa ajili ya uchaguzi.
Masanduku ya kura yakipangwa.
Post a Comment: