Rais wa vyuo vikuu Kenya Ashinda Ubunge uchaguzi Kenya
John Mwirigi.
Aliyekuwa mgombea wa Ubunge Igembe
Kusini nchini Kenya, John Mwirigi (24) ameshinda nafasi hiyo baada ya
matokeo kutangazwa na Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).
Mwirigi ambaye anatajwa kuwa Mbunge
mwenye umri mdogo kuwahi kutokea aliwashangaza wengi katika kampeni zake
ambapo alikuwa akitumia baiskeli na bodaboda.
Mwirigi ambaye ni mwanafunzi wa Shahada
ya elimu katika chuo cha Mount Kenya alikuwa mgombea binafsi hakuwahi
kuwa na matangazo kwa kile kilichodaiwa kukosa pesa za kufanya kazi
hiyo.
Katika matokeo hayo, Mwirigi alipata kura 18,867 huku mgombea wa Jubilee, Rufus Miriti akipata kura 15,411.
Post a Comment: