Polisi wameondoka na Tundu Lissu Mahakamani leo
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa
Singida Mashariki, Tundu Lissu amechukuliwa na Polisi wakati akitokea
Mahakamani akitakiwa Kituo Kikuu cha Polisi baada ya kumaliza shughuli
za Mahakamani.
Tundu Lissu alikuwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwenye kesi ya uchochezi inayomkabili lakini pia alikuwa Wakili kwenye kesi ya Yericko Nyerere.
Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene amesema kuwa wakati gari la Lissu likiwa getini tayari kutoka eneo la Mahakama baada kumaliza shughuli za Mahakama lilisimamishwa na Polisi ambao baadhi walimfuata na kumwambia yuko chini ya ulinzi na kutakiwa kwenda Central Police.

Post a Comment: