Mbunge Ester Bulaya Aruhusiwa Kutoka Muhimbili
Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Amos Bulaya (CHADEMA) ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa akitibiwa tangu wiki iliyopita baada ya afya yake kuimarika.
Bulaya alikamatwa na polisi Ijumaa, Agosti 18 akiwa katika Hotel ya Kifa Best Point Wilayani Tarime mkoani Mara akidaiwa kutaka kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria ambapo aliswekwa rumande.
Hali ya Mbunge huyo ilibadilika ghafla siku iliyofuata baada ya presha kupanda, hivyo kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime ambapo baadaye alihamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo Mwanza, kabla ya kusafirishwa kulazwa wodi namba 18 katika jengo la Sewahaji akipatiwa matibabu.
Amesema afya yake imetengemaa lakini amepewa maelekezo kadhaa.
“Kwanza nitapumzika kwa siku 10, hivyo
ndivyo nilivyoagizwa na nitatakiwa kurudi tena hospitalini kwa ajili ya
kuangaliwa afya yangu zaidi. Kwa sasa nitapumzika kabla ya kurudi
jimboni kuendelea na shughuli za maendeleo,” amesema Bulaya.
Post a Comment: