MAMA SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI UFUNGUZI WA MKUTANO WA 37 WA SADC

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akitambulishwa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 37 wa SADC kwenye ukumbi
wa OR Tambo mjini Pretoria, Afrika ya Kusini. Picha na Ofisi ya Makamu
wa Rais.
Rais
wa Zambia Mhe. Edgar Lungu akiwashukuru washiriki wa mkutano huo wakati
wa Utambulisho kwenye ufunguzi wa mkutano wa 37 wa SADC kwenye ukumbi
wa OR Tambo mjini Pretoria, Afrika ya Kusini.# Picha na Ofisi ya Makamu
wa Rais.
Mkutano
huo wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC
Double Troika Summit),unawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzaia Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Dkt John Pombe Magufuli.Katika mkutano
huo Tanzania itakabidhi nafasi ya Uenyekiti kwa Mwenyekiti mpya.
Double
Troika inahusisha nchi wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland,
Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji. Katika mkutano
huo Mfalme Mswati III wa Swaziland atakuwa ndiye Mwenyekiti. Ajenda kuu
katika Mkutano huu ni kupokea na kujadili taarifa kuhusu hali ya
kisiasa, kiulinzi na kiusalama katika Kanda na hasa nchini DR Congo na
Lesotho.
Mwenyekiti
wa SADC aliyemaliza muda wake Mfalme Mswati III akimkabidhi Uenyekiti
Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa 37
wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa
Afrika mjini Pretoria, Afrika ya Kusini ambapo Tanzania iliwakilishwa na
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais wa Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)
Viongozi
wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika wakiwa
kwenye picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa 37 wa Wakuu
wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika mjini
Pretoria, Afrika ya Kusini .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
…………………………………………………………………………..
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo
tarehe 19 Agosti 2017, amehudhuria ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 37 wa
Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika –
SADC mjiniPretoria Afrika Kusini akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli.
Mhe.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa taarifa fupi kuhusu majukumu
ya SADC Organ kwa kipindi cha Agosti 2016 – Agosti 2017 kwa niaba ya
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa SADC Organ anayemaliza muda
wake.
Makamu
wa Rais amewasilisha kwa Wakuu wa Nchi na Serikali taarifa ya
utekelezaji wa majukumu ya SADC Organ kwa kipindi cha Agosti 2016 hadi
Agosti 2017 kwa niaba ya Mwenyekiti wa SADC Organ anayemaliza muda wake
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Taarifa
hiyo inaelezea hali ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama katika Kanda
katika kipindi tajwa hususan katika Nchi za DRC, Madagascar na Lesotho.Aidha
taarifa hiyo pia imetoa mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto
zinazoendelea kuikabili Kanda katika maeneo ya siasa, ulinzi na usalama.
Taarifa hiyo pia imeelezea hali ya demokrasia na chaguzi zilizofanyika kwa kipindi cha 2016/2017 kwa nchi wanachama.Katika
Mkutano huu Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amekabidhi
Uenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama
kwa Angola, baada ya Tanzania kukamilisha kipindi cha Uongozi wake chini
ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Mkutano
huu wa SADC uliofunguliwa rasmi leo na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini
ambaye ni Mwenyeji wa Mkutano wa 37 wa SADC, ulitanguliwa na mkutano wa
Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili uliofanyika tarehe18 Agosti,
2017
Mkutano
wa Troika Mbiliumefanyika kwa kuzingatia mapendekezo ya Mkutano wa
Mawaziri wa Kamati ya Asasi ya Ushirikiano wa Siasa,Ulinzi na Usalama
(SADC MCO) uliofanyika Dar es Salaam tarehe 20 na 21 Julai, 2017 ambapo
Mawaziri waliona ipo haja ya kuitisha Double Troika pembezoni mwa
Mkutano huu wa 37 ili kujadili pamoja na mambo mengine, hali ya ulinzi
na usalama.
Troika Mbili inahusisha nchi wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji.Serikali
ya Afrika Kusini ambayo ni mwenyeji wa Mkutano huu wa 37 wa SADC na
Mwenyekiti imependekeza kuwakaulimbiu ya Mkutano wa 37 iwe ni
Kushirikiana na Sekta Binafsi katika kuendeleza Viwanda na Kuongeza
Thamani ya Bidhaa.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa Uenyekiti wa SADC kutoka kwa Mfalme Mswati
III, Rais wa Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma amesisitiza nchi wananchama
kutekeleza kwa vitendo Kauli Mbiu ya Mkutano wa 37 wa SADC juu ya
kushirikiana na Sekta Binafsi katika kuendeleza Viwanda na Kuongeza
Thamani ya Bidhaa kuwa ndio njia pekee ya nchi za Jumuiya hiyo kupiga
hatua kimaendeleo.
Rais
Zuma amesisitiza nchi za Afrika kufanyakazi kwa bidii na kuhakikisha
rasilimali za nchi zinatumika kwa faida ya maendeleo yay a kweli.
Wakuu
wa Nchi na Serikali wamepokea taarifa ya utekelezaji wa Mkakati wa
Maendeleo ya Viwanda wa SADC 2015 – 2063 ambao ulipitishwa katika
Mkutano wa Dharura uliofanyika tarehe 29 Aprili, 2015 mjini Harare,
Zimbawe.
Mkakati
huu unalenga kuzifanya nchi za SADC kuwa na uchumi wa viwanda na
kushiriki zaidi katika mnyororo wa thamani kikanda na kimataifa na hivyo
kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi wake.
Mkutano
wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC) utahitimishwa hapo kesho
Jumapili tarehe 20 Agosti 2017, kwa kutolewa Tamko (Communique)
litakaloelezea yaliyojiri katika Kikao cha Wakuu wa Nchi na Serikali.
Imetolewa na ;
Ofisi ya Makamu wa Rais
Pretoria, Afrika Kusini


Post a Comment: