Mahakama ya Rufaa yafuta kesi ya Ugaidi ya Mbunge Wilfred Lwakatare
Mahakama ya Rufaa Tanzania imeyafuta
maombi ya kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ya kutaka kupinga
uamuzi wa Mahakama Kuu kufuta shtaka la ugaidi lililokuwa linamkabili
Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare.
Maombi hayo yamefutwa na Jaji Mussa Kipenka baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Tumain Kweka kueleza kwamba DPP ameamua kuondoa kibali cha maombi hayo kwa sababu hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Kutokana na hatua hiyo Lwakatare ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Usalama wa CHADEMA anakabiliwa na kosa moja la kula njama ya kumdhuru Denis Msacky kwa kutumia sumu ambalo kesi hiyo ipo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Post a Comment: