Thursday, 10 August 2017

Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete, aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowass na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo wameungana na wananchi wa Arusha katika mazishi ya aliyekuwaya mfanyabiashara maarufu, Faustine Melleo Mrema yaliyofanyika Ngurudoto mkoani humo.

 Maelfu ya waombolezaji wakiwemo viongozi wa madhehebu mbalimbali wa dini, wafanyabiashara wakubwa katika sekta ya utalii, wanasiasa, viongozi wastaafu ni miongoni waombelezaji waliomsindikiza tajiri huyo aliyeaga dunia akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini hivi karibuni.

 Mwili wake umepumzishwa katika eneo jipya la makaburi ya familia jirani na hoteli yake ya kitalii ya Ngurdoto Mountain Lodge iliyopo Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.

akizungumza katika mazishi hayo,Mh Edward Lowassa(waziri mkuu mstaafu) wakati wasalamu za pole Mh Lowassa alimzungumzia marehemu kama mtu atakayekumbukwa kwa matendo yake ya kuwajali watu wanyonge.
 

Rais mstaafu Mh Kikwete ambaye hakuzungumza chochote alikua kivutio kwa viongozi na wananchi waliotaka kumsalimia lakini umati wa watu na ulinzi ndiyo vilikuwa vikwazo kwa wananchi huku muda wote akiwa katika hali ya maombolezo.
 Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni waziri wa zamani wa mambo ya nje, Bernard Membe, waziri wa zamani wa fedha, Baziri Mramba, wabunge na wakuu wa wilaya.
 
Askofu Mkuu wa kanisa la International Evangelism, Dk Eliud Issangya aliyeongoza ibada hiyo amemzungumzia marehemu kama mtu aliyewapenda watu wote bila ubaguzi wa rangi wala kabila.

Alisema alikuwa ni mtu aliyependa kufanya kazi kwa bidii, hatua iliyompa utajiri mkubwa ambao aliutumia kuwasaidia wahitaji.
 
 aidha pia Mtoto wa kike wa marehemu, aitwaye Bi Joan Mrema ndiye amepewa jukumu la kusimamia mirathi ya baba yake ambao ni hoteli za kitalii, kampuni za kitalii, maduka ya kubadilisha fedha na biashara nyingine.

Watoto wa Marehemu
Watoto wa marehemu.

Waombolezaji wakiendelea kuaga mwili wa marehemu.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiaga mwili wa mfanyabiashara Faustin Mrema katika ibada iliyofanyika katika hoteli ya Ngurudoto Arusha.


Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowasa akiteta jambo na katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakiteta jambo kwenye msiba wa mfanyabiashara Faustin Mrema


Waombolezaji waliojitokeza katika ibada ya mazishi.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akiaga mwili  marehemu.

Ndugu na marafiki wakiaga mwili.


Ndugu na marafiki wakiaga mwili.

chanzo ;global publishers

Post a Comment: