HAYA NDIO YALIKUA MAAMUZI YA MAHAKAMA DHIDI KESI YA CUF
Mahakama Kuu ya
Tanzania imetupilia mbali maombi ya Bodi ya CUF inayomuunga mkono Katibu
Mkuu, Maalim Seif ya kutaka Msajili wa Vyama vya Siasa asitoe ruzuku
kwa CUF upande wa Profesa Ibrahim Lipumba.
Maombi hayo namba 21 ya mwaka 2017 yametupiliwa mbali na Jaji Wilfred
Dyansobera, baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Gabriel Malata
anayemuwakilisha mdaiwa wa pili Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kusema
kesi imeitishwa kwa ajili ya uamuzi.
Katika uamuzi maombi hayo ambayo mdaiwa wa kwanza ni Prof. Lipumba,
Jaji Dyansobera amesema anakubaliana na moja kati ya pingamizi la AG
kwamba vifungu vya sheria vilivyotumika kufungua shauri hilo sio sahihi.
Hata hivyo, amesema anakubaliana na hoja za Bodi hiyo iliyo upande wa
Maalim Seif kwamba suala la Bodi hiyo kutokuwa na uhalali linahitaji
ushahidi wa kina.
Aidha, kuhusu suala la Maalim Seif kusaini hati mbalimbali za shauri
hilo bila kupewa mamlaka, amesema hilo sio pingamizi kwani Mahakama
haiwezi kutoa uamuzi kwa kuangalia kiapo tu.
”Hivyo mahakama
imetupilia mbali maombi hayo, kwa sababu sheria iliyotumiwa kufungua
maombi hayo sio sahihi, lakini waombaji wanaweza kukata rufaa ama
kufungua kesi nyingine.”
Baada ya kuelezwa hayo, upande wa Maalim wamesema watafungua upya kesi hiyo
Post a Comment: