Ester Bulaya Akamatwa Tena na Polisi
Taarifa kutoka Bunda katika Mkoa wa Mara zinasema kuwa Mbunge wa BUNDA MJINI Mbunge wa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Ester Bulaya kakamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Rorya katika Mkoa wa Mara akiwa katika majukumu ya kichama.
akidhibitisha taarifa hizo msemaji wa CHADEMA, Mh Tumaini Makene: amesema ”Ni
kweli tumepata taarifa muda sio mrefu kwamba Mbunge wetu Jimbo la Bunda
Mjini ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu Ester Bulaya amekamatwa na
Jeshi la Polisi akiwa Hotelini kwake, Tarime. Alikuwa katika shughuli za
kichama akiwa kama Mbunge na Mjumbe wa Kamati Kuu.”
taarifa kutoka JESHI la Polisi Mkoani Mara
zinadai limemkamata Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Esther Amos Bulaya (CHADEMA)
akiwa katika Hotel ya Kifa Best Point Wilayani Tarime akidaiwa kutaka
kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya
Tarime na Rorya, Kamishina Msaidizi Mwandamizi Henry Mwaibambe amesema
wabunge Bulaya na John Heche hawatakiwi kujumuika kwenye mkutano wa
Mbunge wa Jimbo la Tarime.

Post a Comment: