Dk. Kigwangalla aanza ziara ya kikazi Arusha
Naibu Waziri wa Afya, Maemdeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (MB),mapema
leo Agosti 17,2017 amefanya ziara ya kutembelea vituo mbalimbali vya
Afya na kujionea utendaji kazi katika sekta hiyo Mkoani hapa.
Dk.Kigwangalla ametembelea Kituo cha
Afya Kaloleni, kituo cha Afya Levolosi, kituo cha Afya Ngarenaro, Kituo
cha Afya Daraja Mbili, Kituo cha afya Mkonoo na Kituo cha Afya ambacho
kinajengwa cha Muriet Mpya .
Akizungumza wakati wa kutoa maagizo
kwenye vituo hivyo amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dk.
V.Timothi Wonanji na Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha
Dk. Baraka Mundhe na viongozi wengine wa mkoa akiwemo kaimu Mkurugenzi
wa Jiji la Arusha Rebecca Mongi kuhakikisha wanatatua changamoto za
Afya ikiwemo ukosefu wa vyumba vya upasuaji na ukosefu wa vitendanishi
katika mashine za vipimo vya maabara.
“Mnavyo vituo vya Afya 7. Mnahitaji
kuwekeza zaidi ili mnunue vifaa vya Maabara na kufanyia ukarabati hivyo
vilivyopo. Kuna vifaa vya maabara vya kisasa ambavyo ni ‘portable’ na
havina gharana kubwa. Tunataka mtenge fedha za kutosha ili kuimarisha
sekta ya Afya” aliagiza Dk Kigwangalla.
Aidha akitoa agizo wakati kukagua kituo
cha Afya Daraja Mbili ameagiza mara moja jengo la Chumba cha Upasuaji
cha kituo hicho kianze kazi ndani ya wiki mbili na upasuaji ufanyike
ikiwemo wataalamu kuwapo hapo muda wote.
“Naagiza ndani ya wiki mbili. Huduma
za upasuaji zifanyike hapa kwani mnacho kila kitu , vifaa vingi na vya
kutosha na jengo zuri la kisasa” alisema, Dk Kigwangalla.
Katika hatua nyingine Dk.Kigwangalla
ameagiza kituo cha Afya Kaloleni kuhakikisha wanajenga wodi ya akina
mama na kukamilisha maboresho ya Chumba cha upasuaji.
“Hiki kituo hakina hadhi ya kuwa
Kituo cha Afya. Ni sawa na Zahanati tu maana kama hakuna huduma muhimu
za upasuaji na wodi ya wazazi, nahitaji kuona munakamilisha mara moja”
alieleza Dk. kigwangalla.
Katika hatua nyingine, Dk. Kigwangalla
ameweza kukagua sehemu za Maabara, wodi za wazazi na vyumba vya
upasuaji pamoja na maeneo mbalimbali ya hospitali kuona utendaji wa kazi
muhimu na namna ya utoaji wa huduma zinazotolea katika Jiji la
Arusha.
Mbali na kukagua vituo hivyo vya
Arusha, Dk. Kigwangalla pia ameweza kutembelea baadhi ya maeneo
yanayotarajiwa kujengwa vituo vya Afya kwenye maeneo hayo ya Wilaya ya
Arusha.
Naibu
Waziri wa Afya, Maemdeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk.
Hamisi Kigwangalla (MB), akitoa maelezo kwa uongozi wa Kituo cha Afya
Kaloleni namna watakavyojenga wodi ya Wazazi katika moja ya maeneo ndani
ya kituo hicho cha Afya Kaloleni, Wilaya ya Arusha, mapema leo Agosti
17,2017 wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea vituo mbalimbali vya
Afya na kujionea utendaji kazi katika sekta hiyo ya Afya Mkoani hapa.
Naibu
Waziri wa Afya, Maemdeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk.
Hamisi Kigwangalla (MB), akitoa maelezo kwa uongozi wa kituo cha Afya
Levolosi juu ya uwekaji wa vifaa vya Maabara hiyo
Dk. Kigwangalla akkagua chumba cha upasuaji katika kituo cha Afya Levolosi
Dk.
Kigwangalla akikatisha mitaa kwa miguu akitokea kituo cha
Afya Levolosi wakati akielekea kukagua kituo cha Afya cha Ngarenaro
Dk.
Kigwangalla akikatisha mitaa kwa miguu akitokea kituo cha
Afya Levolosi wakati akielekea kukagua kituo cha Afya cha Ngarenaro
Dk.
Kigwangalla akikatisha mitaa kwa miguu akitokea kituo cha Afya
Levolosi wakati akielekea kukagua kituo cha Afya cha Ngarenaro. Kulia
kwake ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dk. V. Timothi Wonanji na kushoto
ni Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Dk. Baraka
Mundhe.
Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha Afya ambacho kinajengwa cha Muriet Mpya wakati wa ziara yake hiyo.
Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha Afya ambacho kinajengwa cha Muriet Mpya wakati wa ziara yake hiyo.
Dk.
Kigwangalla akiwa katika kituo cha Afya Themi wakati wa ziara yake
hiyo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Rebecca Mongi
Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha Afya kinachojengwa wakati wa ziara yake hiyo.
Dk. Kigwangalla akipata picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa sekta ya Afya Jiji la Arusha wakati wa ziara yake hiyo.
Kaimu
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Dk. Baraka Mundhe akitoa
maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla wakati alipotembelea
kituo cha Afya Kaloleni.
Dk. Kigwangalla akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari
Dk.
Kigwangalla akitoa maagizo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Bi.
Rebecca Mongi wakati wa ziara yake hiyo ya kukagua vituo vya Afya
Post a Comment: