*MAHAKAMA LINDI, YAWAACHIA HURU VIONGOZI WA CHADEMA*
Mahakama ya Mkoa Lindi,leo tarehe 01.03.2017 imewaachilia huru,viongozi wa Chadema wafuatao,baada ya kuthibitisha hawakuwa na hatia yoyote,
washitakiwa hao Zeudi Mvano (Makamu Mwenyekiti BAVICHA zanzibar), Namangaya Khamis (Mwenyekiti wa Kanda Mstaafu) ña Philbert Ngatunga (Katibu wa Kanda ya Kusini) walishtakiwa kwa madai ya kuitisha mikutano kinyume cha sheria, hukumu hiyo iliyosomwa na Hakimu Mkazi G. Mhini,ambaye alisema hatua hiyo ilifikiwa baada ya mahakama kupitia ushahidi wa upande wa Jamhuri na utetezi wa viongozi hao ulioongozwa na Wakili msomi Deusdedit Masamaki Kamalamo na kujiridhisha upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kwa ushahidi tuhuma hizo,hatua hii kwa mara nyingine imethibitisha udhaifu wa hali ya juu wa waendesha mashtaka wa serikali,wanaofungua kesi bila kuzingatia sheria kwa shinikizo la Chama cha Mapinduzi
Post a Comment: