Friday, 10 February 2017

Mapema hii leo kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani bungeni na mbunge wa hai M h Freeman Mbowe ameongea na vyombo vya habari.
ikiwa ni siku mbili baada ya mkuu wa mkoa wa dar es salaam kumjumuisha katika moja ya watu wanaotakiwa kufika kituo kikuu cha polisi kati kwaajili ya mahojiana dhidi ya hii vita ya madawa ya kulevya..

Katika press hiyo Mh Mbowe ameongelea mambo makuu matatu.

Moja amekanusha kuhusika kivyovyote vile katika utumiaji wa madawa ya kulevya wala kufanya biashara hiyo haramu.

Pili ni kuitaka jamhuri na viongozi wengine waheshimu mamlaka waliopewa kisheria lakini pia kuheshimu sheria na katiba ya nchii hii.

Tatu amejibu na kutoa taarifa rasmi ya kugomea wito wa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, kwakuwa haujafuata taratibu na muongozo wa sheria za nchi.lakini pia kupinga ushiriki wa uvunjaji wa sheria za nchi maana Mh Makonda hakuwa na mamlaka hayo ya kisheria kutoa wito huo

KATIKA HALI NYINGINE

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Aikael Mbowe (MB) leo tarehe 10 February 2017 amefungua kesi ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu DSM na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dsm.

Kesi hiyo ilisajiliwa kama Kesi ya Kikatiba namba 1 ya 2017 imefunguliwa kwenye Mahakama ya Kuu masijala ya Katiba (Masijala Mkuu).

Kwenye Kesi hiyo Mbowe anaomba Mahakama Kuu itamke na kuwa Mkuu wa Mkoa hana mmalaka ya kudharilisha, na kukamata.
Mbowe pia ameiomba mahakama itengue vifungu vya 5&7 vya Sheria ya Tawala za Mitaa kwakua ni batili na vinakiuka haki za kikatiba.

Katika kesi hizo Mbowe atawakilishwa na Mawakili toka Kurugenzi ya Katiba Sheria na Haki za Binadamu ya CHADEMA.

Post a Comment: