Tuesday, 21 February 2017

Mahakama kuu ya Tanzania leo imeanza kusikiliza kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017, iliofunguliwa na Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Mh Freeman Mbowe.

Katika kesi hiyo Mh Mbowe ameiomba kwanza mahakama itoe zuio la kukamatwa kwake na jeshi la polisi Tanzania kwa madai ya kujihusisha na uuzaji, utumiaji na utengenezaji madawa ya kulevya.lakini kesi ya msingi ni kuitaka mahakama itafsiri mamlaka ya kiutendaji ya wakuu wa mikoa na wilaya na kufutilia mbali mamlaka ya viongozi hao kumeweka ndani mwananchi yoyote kwa masaa 48.

Jopo la majaji watatu wa mahakama hii leo wametoa muongozo wa awali kwa kuitaka jeshi la polisi kusitisha zoezi la kumkamata Mh Mbowe mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa Ijumaa ya Tarehe 24/2/2017

Post a Comment: