YALIOJILI BUNGENI LEO 31/JANUARY 2017
kuapishwa wabunge wapya
Bunge la 11 jamhuri ya muungano Tanzania limeanza leo kwa wabunge mbalimbali amba ni wapya kuapishwa..Mbunge mteule wa Dimani ,Anne Kilango Malecela,Abdallah Bulembo na Professa Palamagamba Kabudi wote wameapa rasmi kulitumikia taifa kama wabunge wa bunge la jamhuri
Kipindi cha Maswali na Majibu
Swali: Serikali ina mpango gani wa kuboresha maslahi ya walimu hasa vijijini?
Majibu: Serikali inaendelea kujenga nyumba za walimu, katika
mwaka 2017/18 serikali inatarajia kujenga nyumba 1818, serikali imelipa
madeni yenye thamani ya shilingi bilioni 20.1. Bado walimu wanadai
madeni ya shilingi bilioni 26.04 ambayo tayari yamehakikiwa. Serikali
inajipanga kulipa deni hilo.
Swali: Ni lini serikali itavipa hadhi vituo vya afya Mirerani na Oleklesh na ni lini serikali italeta gari ya wagonjwa.
Jibu: Maombi ya kupandisha hadhi kituo cha Oleklesh tayari
yamefika wizara ya afya. Halmashauri imetenga gari moja la wagonjwa kwa
ajili ya kuhudumia zahanati mbalimbali za halmashauri hiyo.
Swali: Ni mkakati gani ambao serikali inaweka kuzia tatizo la ulawiti na ubakaji.
Jibu: Sheria inaelekeza kwa mtu anayepatikana na kosa la ubakaji au ulawiti kuhukumiwa miaka 14 jela ila iwe fundisho kwa wengine.
Serikali imeanzisha dawati la jinsia kila wilaya ili kushughulikia
matatizo hayo. Mahakama zimekuwa zinashughulikia kesi hizi kwa haraka
punde ushahidi wa kuridhisha unapopatikana.
Swali: Ni lini serikali itaingilia kutatua mgogoro katika vijiji vya mpanda vijijini?
Majibu: Wizara itaharakisha kutoa ushauri wa kitaalam na kwa kushirikiana na halmashauri ya Mpanda itaanzisha WMA
Swali: Serikali ina mpango gani wa kushusha bei ya maji ktk halmashauri ya Shinyanga?
Majibu: Bei zimepandishwa baada ya kupata kibali kutoka mamlaka
ya udhibiti wa nishati na maji (EWURA). Serikali ina mapango wa
kupunguza gharama ya maji hasa itakapoanza kutumia nishati ya umeme na
jua.
Swali la Nyongeza: Ni lini serikali itaondoa 'service charge' kwenye bili za maji?
Majibu: Tayari imeanza kwa kufunga mita za luku, punde zoezi hilo likikamilika, swala hilo la service charge litakwisha.
Swali: Ni kwanini nguzo za umeme zisilipiwe na serikali ili kurahisisha wananchi kupata umeme?
Majibu: Wananchi hugharamia nguzo za umeme kwa hiyari yao ili
kuharakisha uunganishwaji wa umeme sehemu ambazo TANESCO hawajasogeza
miundombinu hiyo.
Swali: Ni lini serikali itajenga kiwanda cha tumbaku na kusindika asali Tabora?
Majibu: Serikali imefanya na wawekezaji nchini Vietnam na China
ili kuwekeza katika viwanda vya Tumbaku. Kituo cha uwekezaji TIC
kinatakiwa kunadi fursa zilizopo katika uwekezaji ktk mkoa huu.
Chama cha ushirika mkoa wa Tabora wapo kwenye mchakato wa kuanzisha kiwanda cha kuongeza thamani ya tumbaku.
Wananchi wanahimizwa kuanzisha viwanda vidogo kwa ajili ya kusindika asali.
Serikali Imeahidi kuimarisha kazi ya upelelezi na uendeshaji wa mashtaka
kwa lengo la kujenga kesi na kuwa na ushahidi wa kutosha na usiotia
shaka ili kuiwezesha Mahakama kufikia maamuzi ya kuwatia hatiani
watuhumiwa wa vitendo vya ubakaji.
Habari zaidi...
Akijibu swali la mbunge wa Viti maalum Rita Kabati, aliyeuliza nini
mkakati wa serikali wa serikali kunusuru watoto wasiendelee kufanyiwa
matendo ubakaji na ualawiti, na utaratibu gani unatumika kushughulikia
watuhumiwa wa kesi hizo.
Waziri wa Katiba na Sheria mhe. DKT HARRISON MWAKYEMBE amesema serikali
serikali imeanzisha madawati ya Jinsia katika vituo mbalimbali vya
polisi yanayopokea taarifa mbalimbali toka kwa wananchi ili kuwezesha
jeshi la polisi kuendelea na hatua mbalimbali za upelelezi kwa ufanisi.
Amesema katika kufanya uchunguzi wa matukio ya ubakaji serikali
inakabiliwa na changamoto ushahidi kufichwa pale unapohitajika na
wahusika wa pande zote mbili kutokana na kuyamaliza matatizo hayo
kifamilia.
Post a Comment: