BARAZA KUU CUF LAMFUKUZA RASMI UANACHAMA PROF LIPUMBA
Baada
ya msuguano wa kisiasa uliodumu kwa wiki kadhaa baina ya viongozi wa
ngazi za juu katika chama cha Wananchi (CUF) uliosababishwa na kile
kilichodaiwa hujuma za baadhi ya wajumbe kuuvuruga mkutano mkuu wa chama
hicho uliolenga kufanya uchaguzi wa viongozi wa ngazi za juu
uliofanyika mwishoni mwa mwezi Agosti, 2016.
Baraza
Kuu la Uongozi Taifa la CUF, leo limeamua kukata mzizi wa fitina kwa
kumfukuza uanachama Profesa Ibrahim Haruna Lipumba ambae anatuhumiwa
kukivuruga chama hicho.
Baraza hilo liliketi leo kwenye makao makuu ya chama hicho mjini Zanzibar na kufikia maamuzi yafuatayo.
1.
Limemfukuza uanachama, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba baada ya
kujiridhisha kuwa amekiuka katiba ya chama kwa kuvamia Ofisi Kuu ya
chama, kuongoza makundi ya wahuni yaliyopiga walinzi wa chama, kuvunja
ofisi za chama na kufanya uharibifu wa mali za chama siku ya tarehe 24
Septemba 2016.
(Baraza
limejiridhisha kuwa Kikao cha Kamati ya Utendaji kiliitishwa kwa
kufuata masharti ya Katiba na hakikuvunja masharti yoyote ya kuitisha
Baraza Kuu na limejiridhisha kuwa Prof. Lipumba alifikishiwa barua yenye
tuhuma zake lakini kwa makusudi amekiuka kuitikia wito wa baraza na
hivyo kujipotezea haki ya kusikilizwa).
2.
Limeukataa ushauri na mwongozo wa Msajili wa Vyama vya siasa alioutoa
kwa chama kwa sababu umekiuka matakwa ya Sheria ya Vyama Vya Siasa ya
Tanzania, hauna mantiki na mashiko ya kisheria na unakiuka matakwa ya
katiba ya CUF.
3.
Limesisitiza kuwa Kamati ya Uongozi liliyoiunda ndiyo inayotambulika
kikatiba hadi hapo atakapochaguliwa Mwenyekiti mpya wa CUF.
Post a Comment: