ZOEZI LA UHAKIKI VYAMA VYA SIASA LAENDELEA NCHINI
Zoezi
la uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili wa Vyama va Siasa
kwa upande wa Tanzania Bara linaendelea .Tayari vyama 18
vimekwishakuhakikiwa. Vyama vinne vinatarajiwa kuhakikiwa Julai 4.
Zoezi hili ni zoezi la kawaida na endelevu ambalo hufanyika kila mwaka
ili kupima endapo vyama vya siasa vinakidhi matakwa ya Sheria ya
usajili wa vyama vya Siasa.
Uhakiki
wa Vyama vya siasa ni zoezi muhimu sana kwa sababu ni zoezi ambalo
hugusa uhai wa kila chama cha siasa. Kwa upande wa Tanzania Visiwani ,
uhakiki unatarajiwa kuanza mara baada ya kumalizika Bara kwa tarehe
ambazo zitatangazwa baadaye.
Msajili
Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Usajili wa vyama vya Siasa , Bw.
Sisty Nyahoza (kushoto) akihakiki daftari lenye orodha ya wanachama wa
Chama cha NRA (National Reconstruction Alliance) wakati wa zoezi la
kuhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya
Vyama vya Siasa jana Jijini Dar es Salaam.
Msajili
Msaidizi wa Vyama Siasa “Gharama za uchaguzi na Elimu kwa Umma “Bi.
Piencia Kiurea akimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha United
Democratic Party (UDP) Bw. Godluck Ole-Medeye wakati akitoa taarifa
muhimu za chama chake katika zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Kisiasa
unaoendelea Jijini Dar es Salaam.
Msajili
Msaidizi wa Vyama Siasa “Gharama za uchaguzi na Elimu kwa Umma “Bi.
Piencia Kiurea akikagua baadhi ya taarifa za Chama cha Mapinduzi “CCM”
jana wakati wa zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa uliofanyika katika
Ofisi ndogo za chama hicho Jijini Dar es salaam.
Kaimu
Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic Party (DP) Bi. Georgia Mtikila
(kushoto) akitoa taarifa za chama chake kwa Afisa Sheria kutoka Ofisi ya
Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini (kulia), Bi. Jacqueline Kilama wakati
wa zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya
Sheria ya Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam Juni 28 mwaka huu.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Chama cha Jahazi Asilia, Bw. Mbwana S. Kibanda
akifafanua jambo wakati wa zoezi la uhakiki liliofanyika katika ofisi
za chama hicho zilizopo ilala Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mwenyekiti
wa chama hicho na kushoto ni watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama
vya Siasa.
Bw.Eugene
Kabendera, Katibu Mwenezi Taifa wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA)
akitoa taarifa wa watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya
Siasa wakati wa Zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi za chama hicho
zilizopo Jijini Makumbusho Dar es salaam Jana.
Mhasibu
kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw.Willium Brown Nyamtiga
akisisitiza jambo kwa viongozi wa Chama cha Alliance for Democratic
Change (ADC) Jana wakati wa Zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi za
chama hicho zilizopo Jijini Buguruni Dar es salaam.
Bi.
Esther Mwanri, Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
akikagua katiba ya Chama cha Wananchi (CUF) wakati wa Zoezi la uhakiki
uliofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni Malapa Jijini
Dar es salaam. Kushoto ni Bw. Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa uchumi na
Mipango.
Post a Comment: