Monday, 13 June 2016




Baada ya polisi kuzuia kongamano la Bajeti lililokuwa limeandaliwa na chama cha ACT-Wazalendo ambapo kongamano hilo lililenga kumpa fursa ya pekee kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe kusema yale ambayo angeyasema bungeni baada yeye na wabunge wenzake sita wa upinzani kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bajeti bungeni.
Na Baada ya taarifa kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kwamba kiongozi huyo wa chama alikuwa akitafutwa na polisi bila mafaniko leo June 13 2016 amejitokeza mbele ya wanahabari na kuzungumza

Mh Zitto amesema hajui ni kwanini Polisi wamezuia Kongamano lao la Kuchambua Bajeti. Ila nikwamba ''juzi usiku siku ya jumaamosi, watu wetu wa usalama wa chama walinijulisha kwamba Jeshi la Polisi wananitafuta, wakaenda nyumbani kwangu na magari manne kunikamata bila kufuata utaratibu'' wakati Jumanne iliyopita Kamishna Wambura alinipigia kuniomba nifike polisi na nilifika bila kusita hivyo silewi kwanini Hii ya Jumaamosi walikuwa wanataka Kunivizia'
Najua IGP  ameagizwa na MAGUFULI anikamate, lakini hawezi kunikamata bila kufuata utaratibu, hawawezi kunikamata kwa kunivizia, viongozi hatukamatwi kwa kuviwa viziwa, tumewaonyesha na tutawaonyesha kwamba Polisi wanaweza kutukamata kwa kufuata terms zetu na sio zao''
Mpaka sasa chama cha ACT  HaKIfahamu Watawala wanaogopa nini mpaka kuzuia mikutano ya wanasiasa maana tumesikia Jana Walimkamata Mwenyekiti Chadema Huko Mwanza kisa eti kawasalimia wananchi, hakika huu ni uvunjwaji na ukiukwaji mkubwa wa utawala wa kidemokrasia.Hivyo sisi kama ACT Tunalaani kabisa tabia za KIDIKTETA za Rais Magufuli''
''Magufuli ameanza na vyama vya siasa kuonyesha Udikteta wake, nawahakikishia akimalizana na Vyama vya siasa atahamia kwenu Wanahabari, Tumkatalie.na Ndio maana Magufuli Ziara yake ya Kwanza alifanya RWANDA,sasa  tumegundua kuwa alikwenda kujifunza namna ya Kudhibiti Demokrasia na Kuongoza Kidikteta sababu Hauwezi kupambana na UFISADI kama haumpi nguvu ya Kiutendaji wa CAG''
Kwa hali Hii anayokwenda MAGUFULI AJIANDAE KUWA RAIS WA TERM MOJA kwa sababu watanzania hawataweza kuvumilia kutawaliwa, kuminywa na kuburuzwa na Rais DIKTETA KAMA YEYE,Nawasii sana wanaCCM wamdhibiti  haraka na mapema iwezekanavyo Mh MAGUFULI, na wasipomdhibiti sisi na Watanzania Tutamdhibiti
Hatutakaa Kimya hata kama atatufunga, akimfunga Zitto watazaliwa wakina Zitto wengine, na kwenye hili hatutakaa Kimya, tutasimama kidete mpaka nchi irudi kwenye misingi''

Mh Zitto ''amesema Bajeti imeongezeka kwa 32% . ukweli  Je ni kwamba Bajeti imeshuka  na kwa maana Dola imeporomoka.i cha mtu yeyote kufanya kongamano''

Post a Comment: