BUNGE LIMEPITISHA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA YA ELIMU.
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akijibu hoja za Wabunge mapema leo
Bungeni Mjini Dodoma wakati akihitimisha hoja kuhusu muswaada wa sheria
ya marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka 2016.
Naibu
Waziri Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Injinia Stella Manyanya
akitoa ufafanuzi leo Bungeni Mjini Dodoma kuhusu hatua zinazochukuliwa
na Serikali katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wenye ulemavu wanapata
elimu sawa na wale wasio na ulemavu kwa kuweka miundo mbinu rafiki
katika shule na vyuo vyote nchini.
Mbunge
wa Viti Maalum Mhe. Amina Mollel akiuliza swali Bungeni leo wakati wa
kipindi cha maswali na majibu kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali
kuwawezesha wanafunzi wenye Ulemavu sawa na wale wasio na ulemavu hasa
kwa kuangalia miundombinu iliyopo ili iwe rafiki kwa kundi hilo na
kuleta usawa katika kupata elimu.
Naibu
Spika,Dkt. Tulia Ackson akiteta jambo na Mbunge Viti Maalum Mhe. Kiteto
Zawadi Koshuma katika viwanja vya Bunge, mjini Dodoma.
(Picha zote na Frank Mvungi – MAELEZO - Dodoma)
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.
Bunge
la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania leo, Mjini Dodoma limepitisha muswada
wa marekebisho ya sheria ya Elimu kifungu kinachoeleza kuwa mtu
anayempatia ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari kuwa
adhabu yake ni faini isiyozidi shilingi laki tano au kifungo kisichozidi
miaka mitatu.
“Muswada
unapendekeza kuwa kifungu hicho kifutwe na badala yake kitungwe kifungu
kipya cha 60A ili kuweka masharti yanayojitosheleza kuhusu zuio la kuoa
au kumpatia ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari,
kinapendekeza adhabu yake iwe kifungo cha miaka 30 gerezani,” alifafanua
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju.
Vile
vile mtu atakayebainika kusaidia, kushawishi au kuacha mwanafunzi wa
shule ya msingi au sekondari kuolewa au kuoa anatenda kosa la jinai
ambalo adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi milioni tano au kifungo
cha miaka mitano gerezani au vyote kwa pamoja.
Mhe.
Masaju aliendelea kwa kufafanua kuwa, sheria hiyo imependekeza kuwa pale
ambapo kosa hilo litafanywa na mtoto basi adhabu yake itakuwa kwa
mujibu wa masharti ya sheria ya mtoto. Hii ni kwa sababu sheria ya mtoto
inakataza mtoto anayetiwa hatiani kufungwa gerezani.
Aidha
marekebisho hayo katika sheria ya Elimu yanalenga kumjengea mwanafunzi
wa shule ya msingi au sekondari mazingira mazuri ya kumaliza ipasavyo
elimu yake kwa ngazi hiyo.Hivyo basi kila Mkuu wa shule au Mwalimu Mkuu
atawasilisha kwa Kamishna wa Elimu taarifa ya robo mwaka kuhusu matukio
ya ndoa na mimba kwa wanafunzi katika shule yake na hatua
zilizochukuliwa.
Sheria
ya Elimu inamruhusu mwanafunzi aliyepewa ujauzito kuendelea na masomo
mara tu anapojifungua. Sheria hiyo inasubiri kuwekwa saini na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ili ianze
kutumika.
Post a Comment: