Monday, 30 May 2016

*KILICHOJIRI BUNGENI DAKIKA CHACHE ZILIZOPITA*
Naibu Spika kama kawaida yake katoa maelezo ya kile kilichotekea asubuhi ya leo,kuwa ameiagiza kamati ya uogozi kujadiliana na kuleta report yao,hivyo vikao vya bunge viendelee kama ratiba ilivyoonesha.
Mh.John Mnyika alisimama kutaka kuomba muongozo na kunyimwa nafasi hiyo na kiti,hata hivyo baadae naibu Spika aliwaamrisha askari kumtoa  nje kwa nguvu.
Wabunge wa UKAWA waliendelea kupaza sauti juu waziri wa Elimu kuleta maelezo juu ya hatma ya wanafunzi wa UDOM.
Naibu spika alishikiria msimamo na kuwaagiza askari kutoa kambi nzima nje.
Wabunge wa CCM wamesalia ndani kuendelea kijadiri hoja ya maji na si watoto wetu wanaoteseka stand ya mabasi ya UDOM.
 kwasasa Press conference ya UKAWA inaendelea.Na UKAWA yatangaza kutokuwa na Imani na spika,Inaandaa mchakato wa kupiga kura ya kumuondoa madarakani~
Yatangaza kususia vikao vyote atakavyo visimamia

Post a Comment: