TAARIFA KWA UMMA
MAELEZO
YA NAIBU KATIBU MKUU WA CHAMA CHA WANANCHI (CUF), MHE. NASSOR AHMED MAZRUI,
KWENYE MKUTANO MAALUM NA WAANDISHI WA HABARI KWA AJILI YA UZINDUZI WA TAARIFA
YA UVUNJWAJI WA HAKI ZA BINADAMU ZANZIBAR 2015/2106
LAMADA
HOTEL, DAR ES SALAAM – 22 MEI, 2016
UTANGULIZI:
Kipindi cha kuelekea
Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 kilishuhudia kurudi upya kwa matukio ya
uvunjwaji wa haki za binadamu na uhalifu dhidi ya binadamu na utu wao kwa kiwango
kikubwa visiwani Zanzibar.
Matukio haya yalishika
kasi wakati wa uandikishaji wa wapiga kura wapya katika Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura katika miezi ya Aprili hadi Juni 2015, yakaendelezwa wakati wa
kampeni za uchaguzi mkuu na kuibuka tena kwa kiwango cha kutisha baada ya kile kilichoitwa
tangazo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salim Jecha, la
kufuta uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kuendelea hadi sasa.
Uvunjwaji
huo wa haki za binadamu ulihusisha:
1. Kuibuka kwa makundi
ya maharamia ambao wananchi wamekuwa wakiwaita MAZOMBI ambao hufunika nyuso zao
na huku wakibeba silaha za moto na silaha za kienyeji na wakiwa ndani ya gari
zenye namba za Vikosi Maalum vya SMZ wamekuwa wakipiga, kuwaibia mali zao,
kuwajeruhi na hata kuwakata sehemu za miili yao wananchi wasio na hatia katika
maeneo mbali mbali ya visiwa vya Unguja na Pemba.
2. Kuvamiwa kwa
misafara ya wanachama na wafuasi wa CUF waliokuwa wakirudi kutoka kwenye
mikutano ya kampeni na kupigwa na watu waliokuwa wamevalia sare za CCM na huku
wengine wakiwa wamejifunika nyuso zao.
3. Kuwashambulia
wananchi wasio na hatia kwa kutumia risasi za moto kulikofanywa na Polisi na
Vikosi vya SMZ ambako kumepelekea watu kadhaa kujeruhiwa vibaya.
4. Matukio ya ubakaji
dhidi ya wanawake.
5. Unyanyasaji wa kijinsia
dhidi ya mahabusu wanawake waliokuwa katika mikono ya Polisi.
6. Kutekwa watu na
kuwatesa wanapokuwa katika mikono ya watekaji.
7. Kukamatwa ovyo na
kuwekwa ndani kwa watu wasipoungua 90 wakiwemo viongozi waandamizi wa CUF bila
ya kuwafungulia mashtaka Mahkamani kinyume na Sheria za Mwenendo wa Makosa ya
Jinai Zanzibar.
8. Kuwatesa na
kuwaadhibu wanachama na wafuasi wa CUF waliokuwa chini ya mikono ya Polisi
ambao hawakufikishwa Mahkamani huku wakilazimishwa kukiri kutenda makosa ambayo
hawakuyatenda.
9. Kuchoma na kuvunja
ofisi za matawi na majimbo ya CUF pamoja na baraza zinazotumiwa na wanachama na
wafuasi wa CUF kwa kukutana na kubadilishana mawazo.
10. Kuchoma nyumba za
wanachama na wafuasi wa CUF katika vijiji mbali mbali Unguja na Pemba.
11. Kuharibu
miundombinu ya maji na huduma nyengine muhimu za jamii katika maeneo ambayo
yana wafuasi wengi wa CUF.
12. Kuvamiwa kwa kituo
cha redio binafsi na kuwatishia maisha waandishi wanaotangaza vipindi
visivyowaridhisha watawala na kuchoma moto kituo kimoja cha redio binafsi.
13. Kutoa hotuba za
kuchochea fujo, ubaguzi na vitisho kulikofanywa na wanasiasa waandamizi wa CCM
ikiwemo kuruhusu mabango yanayochochea ubaguzi na chuki kwa jamii nzima ya watu
walioitwa “MACHOTARA”.
14. Redio na
Televisheni za Serikali kutayarisha na kurusha vipindi vinavyochochea shari,
fujo na ubaguzi katika jamii.
15. Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kupitia ofisi zake za MASKANI YA KISONGE kuweka ubao maalum unaoitwa
“SAUTI YA KISONGE” unaotumiwa kuandika na kusambaza ujumbe wenye kuchochea
ubaguzi, fujo na ghasia dhidi ya watu wa jamii fulani hasa Wapemba na wanachama
na wafuasi wa CUF.
16. Kuendesha kampeni
za vitisho na kuleta hali ya taharuki na hofu kwa kupitisha askari wakiwa na
silaha nzito nzito pamoja na magari ya kivita katika maeneo yenye makaazi ya
raia visiwani Unguja na Pemba huku wakiimba nyimbo za ubaguzi kwa mfano kusema
“HATUWATAKI MACHOTARA”.
UZINDUZI WA TAARIFA YA
UVUNJWAJI WA ZA HAKI ZA BINADAMU:
Chama Cha Wananchi
(CUF) kimeweka kumbukumbu za matukio yote haya na kimetayarisha Taarifa ya
Uvunjwaji wa Haki za Binadamu ambayo leo hii tutaizindua hapa.
Nimuombe Naibu
Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria, Mhe. Pavu Juma Abdalla, awasilishe
kwenu muhtasari huo wa Taarifa hiyo. Mwisho wa mkutano huu tutawapatia nakala
za Taarifa hiyo kila mmoja.
Baada ya kupokea
Muhatasari huo, niwaeleze kwamba matukio haya na mengine yamechafua sana
taswira na jina la Tanzania katika jumuiya ya kimataifa.
Katika mapitio ya kila
mwaka ya haki za binadamu nchini Tanzania (Universal Periodic Review)
yanayofanywa na Umoja wa Mataifa kupitia United Nations Human Rights Council
ambayo yamefanyika mjini Geneva, Uswisi tarehe 2 – 13 Mei, 2016 yaani mwezi
huu, mataifa kadhaa duniani yaliibana Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusiana
na matukio haya na mengine.
Kiongozi wa ujumbe wa
Tanzania katika mapitio hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof.
Sifuni Mchome, alipata wakati mgumu kujibu hoja hizi.
Rekodi zote za mkutano
huo zinapatikana katika mtandao. Miongoni mwa maazimio yaliyotolewa kwa
Tanzania kutoka mataifa mbali mbali wanachama wa Umoja wa Mataifa ni pamoja na
haya yafuatayo (na nayanukuu kwa Kiingereza kama yalivyoripotiwa kwenye mtandao
http://www.upr-info.org/database/index):
SuR Recommendation RS Response
A Issue
Tanzania ,Africa,AU,
Commonwealth
Ensure that police
officers having committed acts of torture of illtreatment be prosecuted and
punished appropriately
Belgium ,WEOG,EU,
OIF
Accepted
Ø Human
rights violations by state agents
Ø Torture
and other CID treatment
Tanzania ,Africa,AU,
Commonwealth
Take adequate measures
to protect its population from violence committed by the security forces and
establish an independent mechanism for the investigation of complaints
regarding abuses carried out by law enforcement officials
Denmark ,WEOG,EU
Accepted
Ø Human
rights violations by state agents
Ø Justice
Tanzania Africa,AU,
Commonwealth
Establish an
independent body for investigating complaints about the actions of law
enforcement officials
United
Kingdom ,WEOG,EU, Commonwealth
Accepted
Ø Human
rights violations by state agents
Ø Justice
Tanzania ,Africa,AU,
Commonwealth
Provide all victims of
violence against women an unhindered access to justice and ensure that all
perpetrators are brought to justice in accordance with international standards
Slovakia ,EEG,EU
Accepted
Ø Women's
rights
Tanzania ,Africa,AU,
Commonwealth
Improve the efficiency
of the justice system by streamlining and simplifying judicial procedures
including introducing a case management system that tracks individual cases
from filing to disposition and limits the amount of time each case can be held
at each stage
Canada, WEOG, OAS, OIF,
Commonwealth
Accepted
Ø Justice
Tanzania, Africa, AU,
Commonwealth Vigorously prosecute security force personnel who violate the law
United States,WEOG,OAS
Accepted
Ø Human
rights violations by state agents
Tanzania Africa,
AU, Commonwealth
Ensure all security
forces are subject to strict control of civilian authorities
United States, WEOG,
OAS
Accepted
Ø Justice
Tanzania Africa,
AU, Commonwealth
Guaranteeing
the freedom of expression, association and assembly by allowing human rights
defenders, political opponents and journalists to express freely their views in
line with international human rights law
Netherlands -
WEOG EU Accepted 4
Ø Freedom
of association and peaceful assembly
Ø Freedom
of opinion and expression
Ø Freedom
of the press
Ø Human
rights defenders
Ø International
instruments
Tanzania, Africa, AU,
Commonwealth
Work with the media and
other stakeholders to ensure that all organs of the State understand and
appreciate the constitutional guarantees of freedoms of press and assembly
United
States
WEOG OAS Accepted 4
WEOG OAS Accepted 4
Ø Freedom
of association and peaceful assembly
Ø Freedom
of the press
Tanzania, Africa, AU,
Commonwealth
Step
up its efforts to protect women and girls from sexual violence
Norway WEOG
Accepted 4
Ø Rights
of the Child
Ø Women's
rights
Tanzania Africa,
AU, Commonwealth
Work
to abolish laws that restricts freedom of expression, information and freedom
of media, and establish laws that will guarantee these rights in line with
international human rights standards
Sweden ,WEOG ,EU
Accepted 4
Ø Freedom
of opinion and expression
Ø Freedom
of the press
Ø International
instruments
Tanzania ,Africa,AU,
Commonwealth
Respect
the right to assembly throughout the process of reviewing the Constitution
Norway, WEOG
Accepted 4
Ø Freedom
of association and peaceful assembly
Kama inavyoonekana
maazimio yaliyoorodheshwa hapa ambayo pia yanaonyesha nchi gani iliyatoa
yalikubaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Katibu Mkuu
wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome. Yote tuliyoyanukuu hapa
yameripotiwa kwamba ni “ACCEPTED” yaani yamekubaliwa.
Hata hivyo, wakati
maazimio haya na kukubaliwa kwake kukiwa ndani ya mwezi huu huu, bado
tumeshuhudia uvunjwaji wake ukiwa unaendelea.
Matukio ya watu
kuvamiwa katika maeneo yao na kupigwa ovyo yameshamiri upya wiki hii hususan
kisiwani Pemba hasa baada ya ziara ya Katibu Mkuu wa CUF na mshindi wa nafasi
ya Urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015,
Maalim Seif Sharif Hamad ambayo ilikuwa ya mafanikio makubwa.
Tunazo taarifa kwamba
kuna wanasiasa wameliagiza Jeshi la Polisi kuandaa mashtaka kwa ajili ya
kumshtaki Maalim Seif kwamba eti alipokuwa Pemba alifanya maandamano bila ya
kibali wakati hakukuwa na maandamano yoyote.
Tunazo taarifa pia
kwamba kuna njama za kuwakamata tena viongozi mashuhuri wa CUF na hasa Mhe.
Mansoor Yussuf Himid na Mhe. Mohamed Ahmed Sultan (maarufu kwa jina la Eddy
Riyami) na kuwaleta katika magereza ya Tanzania Bara kwa lengo la
kuwanyamazisha Wazanzibari ili wasipaze sauti zao kupinga utawala wa kidikteta
uliowekwa madarakani kwa nguvu za dola kinyume na matakwa ya kidemokrasia ya
wananchi wa Zanzibar.
HATUA TUTAKAZOCHUKUA:
Baada ya hatua ya leo
ya uzinduzi wa Taarifa hii, Chama Cha Wananchi (CUF) kimejiandaa kuchukua hatua
zifuatazo:
1. Kumuandikia
rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Magufuli, na kumkabidhi nakala ya Taarifa hii ili
ajue kinachofanyika nchini na hasa akiwa Amiri Jeshi Mkuu.
2. Kuiwasilisha Taarifa
hii pamoja na vielelezo vyote katika jumuiya, taasisi na mashirika ya kimataifa
yanayotetea haki za binadamu ulimwenguni kwa hatua zao.
3. Kuiwasilisha Taarifa
hii pamoja na vielelezo vyote katika Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
hapa nchini ambayo hata katika mkutano wa Geneva ilitambuliwa uwepo wake, Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar
(ZLSC) pamoja na taasisi nyengine zinazoshughulikia masuala ya haki za binadamu
hapa nchini.
4. Kufungua kesi katika
Mahkama Kuu ya Tanzania dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mkuu wa
Jeshi la Polisi (IGP) kuhusiana na matendo yanayohusisha Jeshi la Polisi
visiwani Zanzibar. Tayari, tokea mwezi uliopita mwanasheria wetu
ameshawasilisha taarifa rasmi kwa Waziri na IGP kuhusu nia hiyo kama sharia
zetu zinavyotaka ikiwa ni hatua ya kwanza katika kufungua kesi hiyo.
5. Kuendelea na hatua
ya kukamilisha taratibu zitakazoiwezesha Mahkama ya Kimataifa ya Uhalifu
(International Criminal Court – ICC) kuanzisha uchunguzi dhidi ya watu wenye
dhamana mbali mbali ambao wamehusika kuchochea, kutoa au kusimamia maagizo
yaliyopelekea makosa dhidi ya ubinadamu na makosa yanayoilenga jamii fulani ya
watu. Jopo la wanasheria wetu limeshaanza kazi hiyo wakiwemo wanasheria wa
kimataifa waliobobea katika kesi za ICC. Tayari kampuni moja ya wanasheria
tuliyoipa kazi hii imeshawaandikia rasmi ICC kuhusiana na suala hili.
MWISHO:
Tunawapongeza na
kuwashukuru wananchi wote wa Zanzibar wanaokandamizwa na kuteswa kwa sababu tu
ya kutetea utu wao na haki zao kwa moyo wao wa ujasiri, ushapavu na uvumilivu
katika kukabiliana na ukandamizaji huu na mateso yanayowakuta.
Tunawahakikishia kwamba
Chama Cha Wananchi (CUF) ambacho wamekiamini na kukipa ridhaa yao kitaendelea
kuwa pamoja nao na kutetea haki zao ikiwemo haki yao ya kuheshimiwa chaguo lao
la kiongozi yupi na chama gani kiwaongoze. Sisi kama viongozi wao hatuna wasiwasi
kwamba kwa mashirikiano ya pamoja HAKI ITASIMAMA NA UTU UTASHINDA.
Ahsanteni kwa
kunisikiliza.
Post a Comment: