KINONDONI KUSIMAMIA MICHEZO KIKAMILIFU ILI KUINUA VIPAJI VYA VIJANA
MSTAHIKI MEYA WA KINONDONI MH BONIFACE JACOB
Manispaa ya Kinondoni i meahidi kusimamia sekta ya michezo kikamilifu ili kuinua vipaji vya vijana katika Manispaa ya Kinondoni.
AFISA ELIMU MANISPAA YA KINONDONI
Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob wakati kufungwa kwa mashindano ya Umoja wa Michezo Sekondari Tanzania (UMISETA) kwa Wilaya ya Kinondoni yaliyofanyika shule ya Sekondari
Makongo leo Jumapili 22/5/2016,ikiwa zimeshirikishwa shule kutoka Majimbo matano ya Dar es salaam.
Akiongea Mstahiki Meya amesema Halmashauri inapambana kurudisha maeneo ya wazi yaliyochukuliwa na matajiri ili vitumike kwa ajili michezo katika kukuza vipaji vya vijana katika Manispaa ya Kinondoni.Amemtaka Afisa elimu Sekondari wa Manispaa ya Kinondoni kuangali viwanja ambavyo vimeharibika achukue greda la Manispaa lipo viwanja vichimbwe ili vijana wacheze kwenye viwanja vyenye hali nzuri.
"Tulikuwa na mazungumzo na waziri viwanja virudishwe kwa wananchi mfano uwanja wa KIFA na UFI, vijana wapate maeneo ya kucheza, tukianza leo kuweka msisitizo katika michezo usishangae 2030 kuwaona vijana wetu wanashiriki kombe la dunia au vipi wanamichezo?" Amesema Mstahiki Meya.
Katika eneo la Mabwepande kuna eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya kutengeneza Sports Centre ya kisasa ambayo vijana watatumia kufanya mazoezi na kucheza michezo mbalimbali, anatafutwa muwekezaji ambae yupo tayari kufanya hilo, akipatikana itakuwa Neema kwa vijana wetu wapenda Maendeleo katika michezo.
Pengine ni Tanganyika Parkers kuna urasimu ulikuwa ufanyike lakini umekwama,imeamuliwa kutakuwa na viwanja viwili vya michezo katika eneo lile.
"Tukiwa serious na michezo na kuandaa na kulinda maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa ajili ya michezo, vijana watapata fursa ya kucheza na kuonyesha vipaji na kuwapatia ajira.
Kinondoni ina miliki timu ya mpira inayoitwa KMC timu ambayo ipo daraja la kwanza, mwaka huu imemaliza nafasi ya pili, timu hiyo haina kocha, haina meneja, Meya amesema hiyo ni fursa ya ajira kwa walimu waliokuwepo hapo, wakipata nafasi hiyo watakuwa kama watumishi wa Halmashauri na kulipwa mishara kupewa mkataba wa mwaka mmoja mmoja na timu hii ni ya wananchi inaendeshwa kwa kutumia kodi za wananchi, timu hii imerudishwa kwa wananchi.Mwezi wa nane ligi inaanza wachezaji watoke Kinondoni Meya amesisitiza.
" Manispaa inatoa motisha kwa timu, kila mchezaji akifunga goli anapewa Shilingi milioni 1,na huwa natoa Milioni 3 kama motisha endapo timu itashinda, timu ina bus la kisasa ambalo huipeleka timu popote katika kushiriki katika mashindano mbalimbali, nategemea kwa siku za mbele KMC itacheza ligi Kuu ya Tanzania,kwa hiyo vijana chezeni kwa bidii mkijua Kinondoni michezo inapewa kipaombele cha hali ya juu" amesema Mstahiki Meya.
Manispaa ya Halmashauri inatoa kiasi cha Shilingi Milioni 100 kusaidia michezo, katika mashindano kulikuwa na timu mbalimbali zikiwemo za mpira wa miguu, netiboli, tennis,vikundi vya ngoma ambapo Mstahiki Meya alikizawadia kikundi cha Ngoma Shilingi 100,000/= taslimu.
WANAFUNZI WA MAKONGO WAKIWA NA VIKOMBE VYAO VYA USHINDI WA MICHEZO MBALIMBALI
Suala la elimu bure ilichanganya kidogo, mwanzoni wananchi walikuwa wakichangia pesa kidogo kwa ajili michezo mashuleni, Manispaa itaangalia ni jinsi gani itaweza kuchangia, Meya Amemtaka Afisa elimu Sekondari wa Manispaa ya Kinondoni kutengeneza bajeti ambayo itasaidia michezo mashuleni, wakati huu Manispaa ilikuwa haijajipanga lakini siku za mbele italitazama hilo kwa undani zaidi kutoka Majimbo matano ya elimu manispaa ya kinondoni, ambapo mshindi ameibuka Makongo Sekondari ambayo itaundwa timu ya kinondoni kushindana na Ilala na Temeke na kupata timu ya pamoja itakayowakilisha mkoa wa Dar es salaam katika mashindano ya UMISETA kitaifa yatakayofanyika jijini Mwanza.
Post a Comment: