ZITTO KABWE: AMJIBU WAZIRI KITWANGA, NA KUDAI SIO ‘SIZE’ YAKE
Wednesday, April 20, 2016
Kiongozi Mkuuwa Chama cha Allience for
Change and Transparency(ACT), Zitto Zuberi Kabwe, ameibuka na kujibu
mashambulizi juu ya taarifa zinazoenezwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Charles Kitwanga kupitia Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) za kumhujumu Rais Dk. Magufuli katika utendaji wake.
Kiongozi huyo amesema anaushahidi wa
moja kwa moja juu ya vitendo vinavyofanywa na Waziri huyo katika kueneza
propaganda zinazolenga kuiyumbisha Serikali ya Awamu ya Nne.
Akasema “Nina
ushahidi usio na mashaka wa Kitwanga kupanga Vijana wanaojiita wa UVCCM
kufanya mikutano na Waandishi wa Habari na anawalipa fedha kufanya
hivyo, nataka ieleweke wazi kuwa nina muunga mkono Rais katika kazi ya
kusafisha Nchi … nitakuwa mtu wa ajabu nisipo muunga mkono katika vita
dhidi ya ufisadi”alisisitiza Kabwe.
Zitto amemtaka Waziri Kitwanga kuepuka
siasa za porojo na kusema waziri huyo si ‘size’ yake na hana mpango wa
kumtoa katika nafasi ya uwaziri hivyo aache kulalamika na kueneza
uzushi.
“Kimsingi
nashangaa mtu kama yeye (Kitwanga) kuweza hata kuwa Waziri wa Wizara
nyeti kama hiyo, zaidi ya yote Waziri Kitwanga sio ‘size yangu’.
Naanzaje kuhangaika na Kitwanga? Ili iweje? Namsihi asijipandishe chati kwamba mimi nataka kumtoa (uwaziri) . Ningetaka kumtoa wala asingejua maana ningeshughulika na aliyemteua” Amesema Kabwe.
Hata hivyo Kabwe amemtaka Waziri
Kitwanga kujipima kama bado anastahili kuendelea kukaa katika nafasi
yake ya uwaziri kutokana na kashfa ya kampuni anayo imiliki iitwayo Infosys kwa
kushirikiana na Kampuni ya Lugumi kuiingizia Serikali hasara ya
shilingi bilioni 34 kupitia Zabuni ya kununua vifaa vya kutekeleza mradi
wa utambuzi wa vidole kwenye Vituo vya Polisi nchini.
“Nawasihi
Watanzania wote kumdharau Waziri Kitwanga nakumtaka ajibu tuhuma
zinazomkabili za kampuni yake binafsi kufanya kazi na Idara katika
Wizara anayosimamia na kwamba ajipime kama anatosha kuendelea kumsaidia
Rais kazi.” Aliongeza Kabwe.
Post a Comment: