Wabunge watakiwa kutanguliza utaifa mbele
Msemaji huyo na CCM, ametoa wito huo juzi wakati akizungumza kwenye mazishi ya aliyekuwa mbunge wa viti maalum (CHADEMA), Christina yaliyofanyika katika kijiji cha Mahambe wilayani Ikungi na kuhudhuriwa na umati mkubwa.
Alisema Christina akiwa mbunge wakati wote hakutanguliza maslahi yake binafsi wala ya chama chake, alitanguliza maslahi ya nchi yake.
“Namjua vizuri Christina kuanzia mwaka 2010 alipoingia bungeni hadi 2015, alikuwa ni mwanamke wa kuaminika, mbunge jasiri, mpole, mzalendo na hakuwa mwanaharakati hata kidogo. Alikuwa akitetea kwa nguvu zake zote…… hoja zenye maslahi au tija kwa taifa letu na hakuwahi kuonyesha chembe yoyote ya itikadi ya kisiasa,” alisema Ole Sedeka.
Akisisitiza, alisema wabunge na hasa wale vijana wajitahidi pamoja na mambo mengine kuachana na uanaharakati, watangulize mbele maslahi ya taifa, ili taifa liweze kusonga mbele kimaendeleo.
Awali mwakilishi wa serikali katika mazishi hayo, Mwigulu Nchemba, pamoja na kutoa pole na rambirambi kwa familia ya Christina Mughwai, aliahidi kumlipia nauli mtoto pekee wa marehemu, Veronica Mukani kurudi masomoni Canada.
Aidha, aliahidi kushirikiana kwa karibu na familia kuhakikisha Veronica anamaliza vizuri masomo yake kwenye Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Newfoundland, St. Johns.
Mwigulu ambaye ni mbunge wa Jimbo la Iramba, aliwavunja mbavu waombolezaji pamoja na Tundu Lissu wakati anamzungumzia marehemu Christina.
Alitania kwa kusema, “Christina alikuwa ni mbunge mpole na mnyenyekevu wakati wote, hali kadhalika na ndugu zake wengine isipokuwa Tundu Lissu Mughwai alipoanza tu kula nyama ya punda, amekuwa mkali kupitiliza”.
Christina Ghwai Lissu Mughwai, alizaliwa katika kliniki ya Ikungi Juni, 21 mwaka 1969 na amefariki Aprili, 7mwaka huu baada kusumbiliwa na maradhi ya kansa. Ni mtoto wa nane kati ya watoto kumi wa familia ya mzee Agostino Lissu Mughwai na Martha Alu Alute.
Post a Comment: