Sunday, 24 April 2016


Aprili 23, 2016  Rais Yower Museveni wa Uganda amemaliza sintofahamu iliyokuwa juu ya nchi gani inastahili kati ya Tanzania na Kenya kujenga bomba la kusafirisha mafuta gafi kutoka Uganda.

Katika Mkutano wa 13 wa Northern Corirodor uliohudhuriwa na viongozi na wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, akiwemo Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Paul Kagame wa Rwanda, Museveni amesema wamekubaliana na Rais Kenyatta kuacha mradi huo uendelee kama ulivyokubaliwa hapo awali ambapo ilikubaliwa kutumika kwa Bandari ya Tanga badala ya ile ya Mombasa.

“Tumekubalina na Rais  Kenyatta juu ya kuuacha mradi huu uendele kama ulivyokuwa hapo awali, hivyo mchakato wa kufanikisha ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania utaendelea kama kawaida”Toka Rais Museven abadili maamuzi ya ujenzi wa bomba hilo kutoka Bandari ya Mombasa nchini Kenya sakata hilo limekuwa likileta mkanganyiko kwa maofisa wa Serikali za Tanzania na KenyaAmbapo mara kadhaa Maofisa wa Serikali ya Kenya wamekuwa wakizozana juu ya uhalali wa kujenga bomba hilo.

Rais Museven alibadili uamuzi wa kujengwa kwa bomba hilo nchini Kenya mara baada ya kukutana na Rais Magufuli wa Tanzania wakati wa mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Arusha.

Katika kikao cha awali baina ya Rais Magufuli na Rais Museven, Rais Magufuli alimuhakikishia Rais Museveni kuwa Tanzania ni sehemu muafaka ya kujengwa kwa bomba hilo, huku kampuni ya Total ikitajwa kukubali kandarasi ya kujenga bomba hilo kutoka Uganda hadi Tanzania

Post a Comment: