Taarifa kwa Umma maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kufanyika 8 Machi, 2016
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto inawataarifu
wananchi wote kuwa tarehe 8 Machi ya kila mwaka Tanzania huungana na
nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku ya Wanawake
Duniani.
Maadhimisho
ya Siku ya Wanawake, hutoa fursa kwa Serikali, wananchi, wadau, na
wanawake wenyewe kupima utekelezaji wa maazimio, matamko na mikataba ya
Kimataifa, Kikanda na Kitaifa inayohusu masuala ya maendeleo ya wanawake
na usawa wa jinsia.
Siku
ya wanawake Duniani husisitiza kujenga mshikamano wa wanawake wote
duniani, kuhamasisha jamii kutafakari kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku
ya Wanawake ya kila mwaka; kuelimisha jamii kuhusu jitihada mbalimbali
zilizofanywa na Serikali na asasi mbalimbali yakiwemo Mashirika Yasiyo
ya Kiserikali katika kuwaendeleza wanawake; na kuhamasisha jamii kuhusu
utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali ya Serikali yenye lengo la
kudumisha Amani, Usawa na Maendeleo.
Post a Comment: