NIDA WAKIRI KUFANYA ‘MADUDU’,SASA WAJIPANGA UPYA..!!
Wednesday, March 02, 2016
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
nchini Tanzania (NIDA) imekiri kwamba vitambulisho vya taifa
vilivyogawiwa havina saini pande zote za nje na na hivyo itautangazia
umma tarehe rasmi ya kuanza kutolewa kwa Vitambulisho vilivyofanyiwa
maboresho na maelekezo kuhusu Vitambulisho visivyo na saini ambavyo vimekwisha gawiwa
Taarifa
kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi
Hati Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwaajili ya kuwataarifu
wananchi na wadau ni kwamba vitambulisho vya Taifa vitakuwa na Saini ya
Mmiliki wa Kitambulisho mbele ya Kitambulisho na Mamlaka ya Kutoa
Vitambulisho vya Taifa (Mkurugenzi Mkuu) nyuma ya Kitambulisho.
Taarifa hiyo imesema kuwa mamlaka hiyo
kwa sasa inafanya jitihada za kurekebisha kanuni, utaratibu na muundo wa
Vitambulisho ili kukidhi mahitaji ya wadau.
Hata hivyo kitengo cha Mawasiliano na
Hifadhi Hati Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesema kuwa
kuweka saini juu ya Vitambulisho vya Taifa kunawezesha utambuzi na
uthibitishaji wa taarifa za mmiliki wa Kitambulisho cha Taifa ambao
haulazimu kutumia alama za vidole.
Vilevile NIDA imewashukuru wadau wote
kwa maoni yao hususani suala la kuweka saini juu ya Vitambulisho vya
Taifa ili kurahisisha utambuzi wa mmiliki wa Kitambulisho na matumizi
mengine ambayo tumeona ni budi kuyafanyia marekebisho.
Aidhaa wadau wote wa NIDA ambao wana
vifaa maalumu vya kusoma taarifa zilizomo kwenye Kitambulisho (Card
Readers) na ambao wameunganisha mifumo yao na Mfumo wa Usajili na
Utambuzi wa Watu wataendelea kutumia njia hizo kuthibitisha taarifa na
utambuzi wa watu.
Post a Comment: