NEC Yateua Wabunge Watatu wa Viti Maalumu
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewateua ndugu Ritha Enespher Kabati na ndugu Oliver Daniel Semuguruka wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na ndugu
Lucy Fidelis Owenya wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa Wabunge Wanawake wa
viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ikumbukwe kuwa Tume katika Kikao chake
cha tarehe 11/11/2015 ilifanya Uteuzi wa Wabunge Wanawake wa Viti Maalum
113 kwa mwaka 2015. Hata hivyo, Wabunge Wanawake wa Viti Maalum
walioteuliwa jumla yake ilikuwa ni 110 kati ya 113 ambapo Viti vitatu
(3) vilibakizwa kusubiri Uchaguzi wa Majimbo nane (8) ambayo Uchaguzi
wake ulihairishwa kutokana na sababu mbalimbali.
Uteuzi wa awali ulihusisha Vyama vitatu
vilivyofikisha asilimia tano (5%) ya Kura zote halali za Wabunge kama
matakwa ya Katiba yanavyotaka. Vyama vilivyopata asilimia tano ambayo
ilikuwa 780,226 ni.
Na. | Jina la Chama | Idadi ya Kura baada ya majimbo 256 kufanya Uchaguzi wa Wabunge |
1. | Chama Cha Mapinduzi (CCM) | 8,332,953 |
2. | Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) | 4,627,923 |
3. | Chama cha Wananchi (CUF) | 1,257,051 |
Baada ya kukamilika kwa Uchaguzi wa
Majimbo hayo nane (8), Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF) ndivyo vilivyoendelea
kupata angalau asilimia tano (5%) ya Kura zote halali za Ubunge, kwa
maana hiyo, vyama hivyo ndivyo vitaendelea kuhusishwa kwenye Mchakato wa
kugawanywa hivyo Viti 3 vilivyobaki.
IDADI YA KURA ZA CCM, CHADEMA NA CUF BAADA YA UCHAGUZI WA MAJIMBO NANE (8) KUKAMILIKA
Baada ya kukamilika Uchaguzi katika majimbo nane (8) Idadi ya Kura kwa Vyama vya CCM, CHADEMA na CUF ni kama ifuatavyo:
Na. | Jina la Chama | Idadi ya Kura baada ya majimbo 256 kufanya Uchaguzi wa Wabunge | Idadi ya Kura baada ya Uchaguzi wa Majimbo nane (8) kukamilika | Jumla ya Kura zote halali za Ubunge. |
1. | Chama Cha Mapinduzi (CCM) | 8,332,953 | 162,535 | 8,495,488 |
2. | Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) | 4,627,923 | 92,958 | 4,720, 881 |
3. | Chama cha Wananchi (CUF) | 1,257,051 | 17,860 | 1,274,911 |
1.0. MGAWANYO WA VITI VITATU (3) VYA WABUNGE WA VITI MAALUM
Kukamilika kwa Uchaguzi wa majimbo nane
(8) kumeonesha kuwa, Viti vitatu vilivyosalia vitagawanywa kwenye vyama
viwili vya CCM na CHADEMA kwa mpangilio ufuatao:
CHAM A CHA MAPINDUZI (CCM)
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge
ilizopata Chama Cha Mapinduzi ni 8,495,488. Hivyo ili kujua Idadi ya
Viti Maalum kitakachopata CCM:
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge
ambazo CCM kimepata unazidisha kwa Idadi ya Viti Maalum vyote na
kugawanya kwa Idadi ya Kura halali za Ubunge kwa vyama vilivyopata
angalau asilimia tano ya Kura zote Halali za Ubunge. Hivyo,
8,495,488 X 113 | = 66.24 ambayo ni 66 |
14,491,280 |
Hivyo, CCM watakuwa na Viti 66 vya Wabunge wa Viti Maalum, awali walikuwa na viti 64.
CHAMA CHA WANANCHI (CUF)
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ilizopata Chama Cha Wananchi (CUF) ni 1,274,911. Hivyo ili kujua Idadi ya Viti Maalum kitakachopata CUF:
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge
ambazo CUF kimepata unazidisha kwa Idadi ya Viti Maalum vyote na
kugawanya kwa Idadi ya Kura halali za Ubunge kwa vyama vilivyopata
angalau asilimia tano ya Kura zote Halali za Ubunge. Hivyo,
1,274,911 X 113 | = 9.9 ambayo ni 10 |
14,491,280 |
Hivyo, CUF wataendelea kubakia na Viti
10 kwa kuwa katika Chaguzi za Majimbo nane (8) hawakuweza kuongeza Kura
ambazo zingewaongezea Idadi ya Wabunge wa Viti Maalum.
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ilizopata Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni 4,720, 881. Hivyo ili kujua Idadi ya Viti Maalum kitakachopata CHADEMA:
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge
ambazo CHADEMA kimepata unazidisha kwa Idadi ya Viti Maalum vyote na
kugawanya kwa Idadi ya Kura halali za Ubunge kwa vyama vilivyopata
angalau asilimia tano ya Kura zote Halali za Ubunge. Hivyo,
4,720,881 X 113 | = 36.81 ambayo ni 37 |
14,491,280 |
Hivyo, CHADEMA watakuwa na Viti 37 vya Wabunge wa Viti Maalum, awali walikuwa na viti 36.
CHAMA CHA WANANCHI (CUF)
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ilizopata Chama Cha Wananchi (CUF) ni 1,274,911. Hivyo ili kujua Idadi ya Viti Maalum kitakachopata CUF:
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge
ambazo CUF kimepata unazidisha kwa Idadi ya Viti Maalum vyote na
kugawanya kwa Idadi ya Kura halali za Ubunge kwa vyama vilivyopata
angalau asilimia tano ya Kura zote Halali za Ubunge. Hivyo,
1,274,911 X 113 | = 9.9 ambayo ni 10 |
14,491,280 |
Hivyo, CUF wataendelea kubakia na Viti
10 kwa kuwa katika Chaguzi za Majimbo nane (8) hawakuweza kuongeza Kura
ambazo zingewaongezea Idadi ya Wabunge wa Viti Maalum.
MAPENDEKEZO YA MAJINA YA UTEUZI WA VITI MAALUM KWA VYAMA VYA CCM NA CHADEMA
Tume hufanya uteuzi kwa kufuata
mtiririko wa orodha iliyowasilishwa na Katibu wa Chama husika, kwa
mantiki hiyo Tume imewateua Wabunge hao kama ilivyojitokeza katika
orodha za Vyama vya CCM na CHADEMA.
Katika orodha iliyowasilishwa na CCM majina nambari 65 naa 66 ni
- Ndugu Ritha Enespher Kabati
66.Ndugu Oliver Daniel Semuguruka.
Katika Orodha iliyowasilishwa na CHADEMA jina nambari 37 ni
- Ndugu Lucy Fidelis Owenya.
Post a Comment: