MH LEMA : CCM IMEJAA UHUNI NA UBABE UBABE
Kupitia ukurasa wake wa
Facebook Godbless Lema amesema kitendo cha polisi kuwakamata wabunge wa
Chadema na kuwaweka ndani wakati uchaguzi wa Halmashauri ukiendelea ni
mbinu waliyotumia CCM ili kupunguza kura za wajumbe hao, jambo ambalo
limepelekea UKAWA kushindwa ili hali wao walikuwa na wajumbe wengi zaidi
ya CCM.
"Leo ilikuwa siku ya
Uchaguzi Halmashauri ya Kilombero baada ya kuahirishwa mara kadhaa.
UKAWA ina wajumbe 20 na CCM 19. Hii ina maana kuwa UKAWA tulikuwa na
uhakika wa kushinda na kuongoza Halmashauri hiyo. Baada ya CCM kujaribu
kuwahonga madiwani kadhaa na kushindwa kufanikisha lengo lao, leo
wakabuni mbinu mpya ya kishetani. Wakamkamata Mbunge wa Kilombero Peter
Lijualikali na Mbunge wa Viti Maalum Devotha Minja na kuwaweka mahabusu
huku uchaguzi ukiendelea" Aliandika Godbless Lema
Kufuatia jambo hilo Mbunge huyo amesema kuwa jambo hilo ni jambo ambalo halivumiliki kwani ni ukatili, ubabe na uhuni
"Kwa kufanya hivyo wakawa wamepunguza kura 02 za UKAWA (kura ya Lijualikali na ya Devotha). So UKAWA ikabaki na madiwani 18.
Uchaguzi umefanyika CCM
wameshinda kwa kura 19 na CHADEMA 18. Huu ni ubabe, uhuni na ukatili
usiovumilika. We must take action. Haiwezekani tuhujumiwe kwa kiasi hiki
halafu tukae kimya. Huu ni ubabe ambao hata Shetani hawezi kuufanya.
Tusipochukua hatua wataendeleza ubabe huu wa kijinga. Watafanya hivyo pia kwa Dar" Aliongeza Godbless Lema.
Post a Comment: