Dkt Shein aongoza Wazanzibar kupiga kura uchaguzi wa Marudio leo
Sunday, March 20, 2016
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa
Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein
amewaongoza wazanzibar katika zoezi la upigaji kura mapema leo Machi
20.2016 linaloendelea visiwani Zanzibar katika uchaguzi wa marudio
ambapo amejitokeza kupiga kura katika kituo nambaa moja katika skuli ya
Msingi Bungi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Uchaguzi wa leo ni wa marudio baada ya kufutwa kwa uchanguzi uliofanyika October 25,2025 kutokana na kasoro zilizojitokeza.
Makamu
wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi
akizungumza na baadhi ya Waandishi wa Habari mara baada ya kupiga
kura katika uchaguzi wa marudio kwenye kituo cha Skuli ya Kitope, Wilaya
ya Kaskazini B , Mkoa wa Kaskazini.
Baadhi ya Wakazi wa Madungu wakiangalia majina yao kwenye kituo cha kupigia kura
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa
Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein
akipiga kura katika uchaguzi wa marudio kituo namba 1cha kupiga kura
namba 1 Skuli ya msingi Bungi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
leo.
Post a Comment: