Thursday, 24 March 2016


Dkt. Ali Mohamed SheinJaji
Mkuu wa Zanzibar, Jaji Omary Othman Makungu (kulia) akimuapisha Dkt.
Ali Mohamed Shein kuwa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa mujibu wa
katiba katika Uwanja wa Amani mjini Unguja leo.
Rais Mteule wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein ameapa kuwa Rais kwa mujibu wa katiba
katika kuongoza wananchi wa Zanzibar kwa muda wa miaka 5.


Rais Mteule ameapishwa na Jaji Mkuu wa
Zanzibar Jaji Omary Othman Makungu mbele ya viongozi wa nchi pamoja na
viongozi wa dini na kushuhudiwa na mamia ya wananchi katika uwanja wa
Amani mjini Unguja.


Baada ya Rais Shein kuapishwa viongozi
wa dini wameomba dua wakiongozwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh
Khamis Haji Khamis na kufuatiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo
la Zanzibar Mhashamu Augustino Shayo na Askofu wa Anglikana Dayosisi ya
Zanzibar Padre Michael Henry Hafidh.


Viongozi mbalimbali wamehudhuria Kiapo
hicho akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
viongozi wastaafu wa kitaifa na mamia ya wananchi.


Aidha Rais Dkt. Ali Mohamed Shein
ameapishwa na kuwa Rais wa awamu ya saba kwa serikali ya mapinduzi ya
Zanzibar na kukagua gwaride rasmi, pamoja na itifaki nyingine kufuatia.
 
Rais Shein Akila Kiapo

Post a Comment: