Breaking newz:huu ndio mpango mkakati wa Ccm kununua umeya Dar
Habari zilizotufikia hivi punde kutoka kwa mpekuzi wetu.baadhi ya wajumbe wa Chama cha Mapinduzi ( CCM ) wakiongozwa na Mh Angela Kairuki pamoja na Mh Madabida.siku ya leo walikuwa na mkutano wa siri uliofanyika Lamada Hotel,Ilala.
Kikao hicho ni maalumu kwa ajili ya kupanga mkakati wa kushinda uchaguzi wa umeya wa jiji la Dar es salaam.ambapo kwa pamoja wameafikiana kuwa mkakati wa kwanza ni kuwanunua madiwani wanaotokana na umoja wa UKAWA Kwa kiasi kisichozidi mil 25 za kitanzania kwa Kila mmoja.katika kutekeleza hili wameunda kamati inayoongozwa na Mh Kessy,diwani wa Kata ya Kisutu na Mh Sultan,diwani wa upanga magharibi kutekeleza mpango huu
kutokana na hili blog ya siasa leo tz kwa niaba ya wakazi wa Dar na Tanzania tunaitaka TAKUKURU wafuatilie mienendo ya watu hawa.sambamba na mwenendo Mh Songoro, Diwani wa kata ya Mwananyamala pamoja na madiwani wenzie wa Ukawa, ambao tayari wameshiriki dhambi hii ya usaliti .na sisi wananchi hatukubaliani nayo, kwa sababu inapoka mamlaka halali ya wananchi.Kubwa zaidi ni Meya wa Temeke Mh Chaurembo kuhakikishia kikao hicho kuwa kura za viti maalum kutoka halmashauri ya Temeke aachiwe jukumu hilo kwakuwa anawamudu.
Pia tunamuomba Mh rais John P Magufuli kulifanyia kazi hili suala la rushwa na ulanguzi wa mamlaka ya umma unaofanywa na baadhi wa wajumbe wa chama chake kwa niaba ya kamati kuu.lakini swali kujiuliza hapa ni nini hasa CCM na Mh MADABIDA wanafaidika na umeya wa jiji la Dar es salaam kiasi cha kukubali kuununua kwa gharama kubwa namna hii !? Hakika hili ni jipu ambalo Mh rais yakupasa kulitumbua haraka.
Post a Comment: