Wednesday, 24 February 2016




Wakazi wa mji wa kinondoni,jijini D ar es salaam hivi karibuni wataanza kunufaika na utawala mpya wa meya kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA ).Akiongea na wananchi pamoja na waandishi wa habari hivi karibuni Meya huyo wa  halmashauri  ya  manispaa  ya  kinondoni  Mh Boniface Jacob , amesema “ mkakati wa kwanza walionao wao kama halmashauri chini ya utawala wake ni kuwaondoa wakazi wa kinondoni katika dimbwi la hali duni ya maisha ilhali kinondoni ndio wilaya inongoza kwa mapato Tanzania .katika kusapoti mkakati huo wa halmashauri Mh BONIFACE JACOB  ameanza kwa kufuta  bajeti ya viburudisho  kwenye ofisi yake ya meya wa kinondoni badala yake kuzielekeza pesa hizo huko kwenye ujenzi wa barabara mbalimbali zilizo chini ya uangalizi wa halmashauri yake .
 “inaumiza kuona wananchi wako wakiangaika sehemu za biashara na kazi za kufanya halafu wewe kama kiongozi unajiwekea bajeti ya mamilioni kwa ajili ya viburudisho ofisini !!”
mimi kama Boniface Jacob na chama changu cha CHADEMA pia umoja wa UKAWA hatukubaliani na mfumo huo kandamizi.
          Mh Boniface Jacob-Meya wa Kinondoni

Akifafanua zaidi Mheshimiwa meya amesema
Pamoja na hilo halmashauri tayari imetenga kiasi cha pesa tsh bilioni 2.5 kwajili ya kutengeneza vibanda vya matoroli ya kisasa kwa ajili ya biashara ndogondogo za machinga ambavyo vitagaiwa kwa wananchi kwa ajili ya kuendesha maisha yao. Nia na maudhui ni kuona kinondoni inazidi kusonga mbele kama halmashauri inayojitegemea kwa mapato yake ya ndani wanaokusanya lakini pia wakazi wake wakishirikishwa ipasavyo katika mchango wa kuendeleza wilaya yao.
Manispaa ya kinondoni ina vyanzo 46 vya mapato,na inaweza kukusanya mapato ya kiasi cha bilioni 46 ,ni wilaya tajiri sana sema serikali ya CCM walikua wanaifuja hovyo”
Pia mh meya amesisitiza kuwa tayari kuna mpango mkakati unaondelea baina ya halmashauri na benki ya DCB ili kuwawezesha kina mama na vijana wa wilaya ua kinondoni  kwa kuwakopesha mitaji midogo midogo na yenye riba nafuu ili waende kuanzisha biashara mbalimbali .katika kuhakikisha hili linafanikiwa halmashauri wameshatoa takribani milioni 200 kwenda kwenye benki hiyo ya maendeleo ya mkoa wa Dar es salaam (DCB)

Post a Comment: