Uchaguzi Marekani, Trump Agaragazwa na Ted Cruz
IOWA, MAREKANI
Seneta wa Texas Ted Cruz ameshinda mchujo
wa mgombea wa uchaguzi kupitia Chama cha Republican katika jimbo la
Iowa, Marekani. Huo ndio mchujo wa kwanza katika uchaguzi wa urais wa
2016 ambao utafanyika baadaye mwezi Novemba. Cruz amepata asilimia 28 ya
kura.

Donald Trump
“Huu ni ushindi wa wahafidhina jasiri,” mgombea huyo amesema baada ya
kubainika kwa ushindi wake. Mfanyabiashara Donald Trump alikuwa
akiongoza kwenye kura za maoni kabla ya kura kupigwa lakini sasa amekuwa
wa pili akipata asilimia 24 ya kura zilizohesabiwa.
Seneta wa Florida Marco Rubio amefanya vyema kuliko ilivyotarajiwa
amekuwa wa tatu akipata akipata asilimia 23 ya kura zilizohesabiwa.
Kura za mchujo wa chama cha Democratic bado zinahesabiwa.
Asilimia 85 ya kura ambazo zimehesabiwa zinaonyesha pengo kati ya Hillary Clinton na mshoshialisti wa Chama cha Democratic, Bernie Sanders ni 1% pekee.
Asilimia 85 ya kura ambazo zimehesabiwa zinaonyesha pengo kati ya Hillary Clinton na mshoshialisti wa Chama cha Democratic, Bernie Sanders ni 1% pekee.
Akizungumza baada ya matokeo kujulikana, Marco Rubio amempongeza Bw
Cruz na kusema ndiye mgombea ambaye anaweza kuunganisha chama cha
Republican ambacho kimegawanyika.
Dakika chache baadaye, Bw Trump alipanda jukwaani katika ukumbi
mwingine na kumpongeza seneta huyo wa Texas, na kusema anaridhika
kumaliza katika nambari mbili.
Wagombea wawili wamejiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho.
Wagombea wawili wamejiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho.
Upande wa Republican, gavana wa zamani wa Arkansas Mike Huckabee ameandika kwenye Twitter kwamba atasitisha kampeni yake.
Post a Comment: