SHEIKH PONDA AZUNGUMZIA UCHAGUZI ZANZIBAR
Katibu
wa Jumuia na Taasisi za kiislam Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda,
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana na kutoa msimamo
wa Jumuia ya Kiisalam,u na Taasisi zake kuhusiana na suala la uchaguzi
wa Zanzibar na kumuomba Rais John Magufuli kuingilia kati suala hilo.
*********************
KWA
mara ya kwanza tangu atoke mahabusu, Katibu wa Jumuia na Taasisi za
kiislam Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda amezungumza na vyombo vya
habari na kukanusha taarifa ya za kiongozi wa Uamsho kuunga mkono
uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar.
Juzi
akizungumza na vyombo vya habari, Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad
Salum, alisema amepokea barua kutoka kwa Amir wa Uamsho, Sheikh Farid
Hadi Ahmad ambaye yuko gerezani, akieleza kuunga mkono suala la kufanya
uchaguzi wa marudio kwa kuwa ndiyo njia pekee ya kumaliza mgogoro huo,
na kuwa hakuna njia mbadala.
Shehe Ponda alisema kuwa Shehe Farid amewatuma kukamnusha madai hayo na kuwa yeye hajamtuma mtu yeyote kuzungumzia suala hilo.
“Tumemtembelea
Shehe Farid gerezani, lakini pia tulikutana na wanasheria wake pamoja
na viongozi wa gereza kutaka kujua kama aliandika barua yeyeyote na si
yeye wala mwanasheria au magereza waliothibitisha kufanya hivyo nae
kutuomba kukanusha taarifa hizo na kusema hazina ukweli wowote,” alisema
Shehe Ponda.
Ponda
amemtaka Rais John Magufuli kutekeleza ahadi yake aliyoitoa Bungeni juu
ya kufuatilia hatma ya hali ya kisiasa visiwani Zanzibar na kutoa tamko
la yale yaliyofikiwa katika mazungumzo ya kutafuta suluhu yaliyokuwa
yakihusisha pande mbili zinazo vutana za Chama cha Wananchi CUF na Chama
cha Mapinduzi (CCM).
“Rais
achukue ahadi yake aliyoitoa Bungeni, anawajibu wa kuitekeleza kwa
vitendo na ahakikishe mzozo huu anaupatia ufunbuzi bila ya kuitumbukiza
Zanzibar kwenye dhiki na uhasama,” alisema Ponda
Pia
alisema kuwa vyombo vya usalama vilivyopo Zanzibar vipo kwa amri yake
hivyo ebndapo patatokea jambo lolote kabla ya kumaliza mzozo wa kiauisa
uliopo visiwani humo ni yeye atakae laumiwa.
Aidha
akizungumzia kuhusu uchaguzi Mkuu wa Zanzibar iliofanyika Oktoba 25
mwaka jana nchini kote ukisimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na
Ule wa Zanzibar uliosimamiwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na
kasha ZEC kufuta matokea yake na kutangaza kurudiwa tena Machi 20 mwaka
huu, kuwa uchaguzi huo ulikuwa mzuri na halali huku NEC na ZEC
zikifanya kazi yao vizuri.
“Uchaguzi
wa Oktoba 25, 2015 kwa pande zote za Muungano uliosimamiwa na NEC na
ZEC ulikuwa halali na mchakato wake kwa ujumla ulikwenda vizuri kwani
Rais wa Muungano Wabunge, Madiwani, wawakilishi wamepatikana kwa
uchaguzi huo, Sehemu ya Zanizbar Wabunge wa Bunge la Muungano pia
wamepatikana kwa uchaguzi uliosimamiwa na ZEC na matokeo yake
tunayaheshimu,”alisema Shehe Ponda.
Ponda
alisema kuwa wao kama Jumuia na Taasisi za kiislam wanaungaa mkono
hatua za mwanzo zilizochukuliwa kunusuru hali ya kisiasa Zanzibar kwa
kufanya mazungumzo baina ya vyama hasimu vya CUF na CCM pamoja na kuunga
mkono ahadi ya Rais John Magufuli ya kushughulikia mzozo huo aliyoitoa
Bungeni.
Amehoji
ukimya uliopo hadi sasa kwani watanzania hawajapewa taarifa ya pamoja
kutoka CCM na CUF kuhusiana na mazungumzo waliyofanya yameishia wapi na
yapi wamekubaliana na yapi hawajakubaliana na nini hatima ya mazungumzo
yao.
Ponda
alisema kuwa Jumuia na Taasisi za kiislam inapinga vikali uamuzi wa ZEC
kutangaza tarehe ya kurudia uchaguzi kabla ya ufumbuzi wa mambo ya
msingi na ya kisheria kupatikana kwani hatua hiyo inaweza kuleta fujo na
uhasama na kuharibu utangamano uliopatikana kwa kipindi cha miaka ya
karibuni Zanzibar.
Katika
hatua nyingine Msemaji wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Rajabu
Katimba amesema kuwa vyama vya siasa, Msajili wa vyama vya siasa na
wananchi wote wakemee na CCM ifute kauli na kuwaadhibu wanachama wake
waliotoa kauli za kuwa CCM Zanzibar ahitatoa serikali kupitia sanduku la
kura (karatasi) kwani ni nchi ya Mapinduzi na pia kauli za kibaguzi
ilizotolewa kwa njia ya mabango hivi karibuni.
Post a Comment: