MEYA WA KINONDONI AMUONYA DC MAKONDA ACHE UTAPELI
MEYA WA MANISPAA YA KINONDONI MH BONIFACE JACOB
MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni,
Boniface Jacob amemuonya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kuacha tabia
ya kuingilia majukumu ya Halmashauri, badala yake afanye kazi zinazomuhusu.
Pia alisema uingiliaji huo ni utapeli uliomsababisha Rais
John Magufuli kuagiza kila waziri akatwe Sh. milioni moja katika mshahara wake,
pamoja na yeye mwenyewe, Waziri Mkuu Kassim Majalaliwa na Makamu wa rais Samia
Suluhu Hassan kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa madarasa na shule mpya katika
Jiji la Dar es Salaam.
Rais Magufuli alifikia uamuzi huo alipokuwa
akizungumza na Taifa kupitia mkutano wake na Wazee wa Dar es Salaam, baada ya kuelezwa
matatizo ya ongezeko la wanafunzi wa darasa la kwanza katika mkoa huo,
lililotokana na utekelezaji wa ahadi ya elimu bure.
Akizungumza jana jijini Dar
es Salaam, Meya Jacob (Chadema) alisema ameradhimika kumuonya DC Makonda
kutokana na tabia ya kutafuta sifa ili aonekane mchapakazi, hali ya kuwa ana
dandia kazi zisizomuhusu.
Alisema hakuna sheria
inayomruhusu Makonda kushirikiana kikazi na Halmashauri hadi awasilishe barua
ya maombi kwa Mkurugenzi ama Meya kama anahitaji kufanya jambo lolote.
Majukumu
Jacob alisema ma-DC nchini
wana majukumu muhimu matatu tu, ikiwemo Uenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama, Uenyekiti wa Kamati za Mashirikiano pamoja na kuwa Kiunganishi wa
Serikali ya Mtaa na Serikali Kuuu.
Kuhusu wenye uwezo wa
kuzungumzia maswala ya Halmashauri, Jacob alisema ni watu watatu wenye mamlaka
ambao ni Mkurugenzi, Meya na Afisa Habari lakini si DC kwa kuwa haimuhusu.
“Kitu kilichosababisha
nieleze haya na kutoa ufafanuzi huu ni kutokana na kitendo alichokifanya
Makonda hivi karibuni kuueleza umma kwamba Halmshauri ya Kinondoni imepokea USD
300 kutoka Benki ya Dunia (WB) kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara
hali ya kuwa hakupaswa kulizungumzia kwani lipo nje ya uwezo wake,
Ilikuwa bado ni taarifa ya
siri lakini akaidukua na kukurupuka kuitangaza, jambo ambalo limesbabisha
mtafaruku mkubwa kutoka kwa wajumbe wa Baraza la Madiwani wakihoji kwanini
taarifa hizo zitolewe bila ya kamati kupitisha,’alisema.
Jacob alisema kutokana na hatua
hiyo, wanamtaka Makonda kutoingilia majukumu yasiyokuwa yake;
“DC hana uwezo wa kupanga
bajeti wala kutoa fidia ama kuzungumzia kitu chochote kinachosu Halmshauri hadi
aombe ruhusa, pia hakuna mahusiano yoyote baina ya DC huyo na Halmashauri,”alisema
Pia alisema walimvumilia DC
kutokana na vitendo vyake lakini kwa sasa wamefikia mwisho na wanamuonya kuacha
tabia za udukuzi.
Utapeli
Kuhusu utapeli huo wa
Makonda kwa Rais Magufuli alisema kuwa Halmashauri hiyo haina shida ya msaada
wowote kutoka kwenye mshahara wa rais.
Alisema halmshauri hiyo inakusanya
takribani sh.bilioni 46 kwa mwaka, huku ikipata kiasi cha sh.bilioni 78
ikijumuiha na mishahara ya watumishi, ambapo kwa mwaka inapata sh.bilioni 152.
“Hatukupenda rais atangaze
kukata mshahara wake kwa kuwa hatuna shida nao, kama ingekuwa uwezo wetu
tungeamuandikia barua asikate bali uende kusaidia Halmashauri ya Ilala na
Temeke lakisi sio kwetu,”alisema.
Alieleza kuwa hatua hiyo
inatokana na halmashauri hiyo kuwa na pato kubwa isipokuwa lilikwamishwa na uongozi
wa Chama cha Mapinduzi (CCM), uliopita kwa kufanta ubadhirifu wa fedha.
“Mathalani kuna kigogo wa
CCM alikuwa anafanya kufuru kwenye ulipaji kodi wa mabango madogo, ambapo
tukikusanya kodi zote za mabango kama inavyotakiwa tunapata zaidi y ash.bilioni
10 kwa mwaka,
Ni aibu kuona DC
anahangaika na maombi ya msaada kama omba omba hali ya kuwa Halmashauri ina
uwezo mkubwa, alitakiwa aje kutuomba ili tumsaidie lakini sio kukimbilia
udukuzi ili aonekane anafanyakazi kubwa,”alisema.
Hofu
Jacob alisema kutokana na
udukuzi wa Makonda kuhusu taarifa za utekelezaji wa mradi huo, kwa sasa wajumbe
wa Kamati ya Fedha wana hofu dhidi ya Baraza la Madiwani kwa kuwa taarifa zimevuja
kabla ya kukaliwa kwa vikao halalali.
Alisema kwa mujibu wa Kanuni
za Halmashauri namba 8 ya mwaka 1982 hairuhusiwi mtu yoyote akiwemo Meya na
Mkurugenzi kuzungumzia suala la vikao vya halmashauri nje ya vikao, lakini
Makonda amediriki kufanya hivyo.
“Siku zote Mgema akisifiwa Pombe huitia maji,
ndio haya anayoyafanya Makonda baada ya kusifiwa na rais kila kazi anajiona
anaweza kuifanya ili apate sifa wakati anashindwa kujua baadhi ya vitu si
jukumu lake wala havimuhusu,’alisema.
Alisema taarifa za mradi huo
(DMDP) zilizosambazwa na Makonda hazikupangwa kwa Kinondoni pekee bali ni mradi
uliolilenga jiji la Dar es Salaam, kuwa kama miji mingine mikubwa Duniani
ikiwemo Paris Ufaransa, ambapo kuzungumziwa tangu mwaka 2014.
Pia alisema Manispaa
imeingiwa na mtanziko kwani Kamati ya Baraza limeanza kuhoji uhalali wa Makonda
kuhusu udukuzi huo, hivyo kuna uwezekano wa kupingwa kwa matumizi ya fedha hizo
kwenye vikao vya baraza.
“Pia ameibua hofu kwa
wananchi wa Bonde la Mto Ng’ombe kwamba watavunjiwa nyumba, hali ya kuwa
halmashauri ilishaweka utaratibu wa kuwalipa fidia wananchi hao takribani sh.bilioni
1.7, huku waliokuwa pembezoni mwa barabara zitakazopitiwa na mradi huo
watalipwa sh. bilioni 14,”alisema.
Shule
Kuhusu ujenzi wa Shule za
Sekondari ambapo Makonda alitangaza arambee ya uchangiaji Saruji, Jacob alisema
anachofanya Makonda ni uongo kwa kuwa sio mjumbe wa Baraza la Madiwani kwani hakupaswa
kulizungumzia.
“Tangu apokee mifuko ya
Saruji hadi sasa hakuna hata mmoja uliopelekwa kwenye shule, anacofanya ni
utapeli tu inatakiwa tujiulize kaipeleka wapi labda iwe kwenye ofisi za CCM,”ALISEMA.
Pia alisema Makonda hana
uwezo wa kumfukuza hata mfanyakazi wa kufagia katika ofisi za Halmashauri, wala
kubanga bajerti ya sh.5000 au kumuwajibisha mtu yoyote kwa kuwa sio ujukumu
lake kiutawala wala kisheria.
Hatua
Jacob alibainisha kuwa
kutokana na kumuonya mara kadhaa DC huyo endapo akiendelea kufanya udukuzi basi
watawaondoa Maafisa tarafa kwenye vikao vya Baraza la Madiwani ambao wamekuwa
viunganishi wake,
“Kwa kuwa mihimili hii ni tofauti
siwezi kumpigia simu Makonda kumuuliza kwanini amezungumzia hayo bali anatakiwa
anitafute baada ya kusikia nimeongea haya,’alisema.
MWISHOOOO.

Post a Comment: