KAMANDA SIRO KUPIGA MARUFUKU MAANDAMANO YA CHADEMA
Jeshi la Polisi kanda
Maalumu Dar, limepiga marufuku maandamano ya Vijana wa CHADEMA kwenda
Ikulu kwa lengo la kushinikiza TBC ionyeshe Bunge LIVE.
Kamanda Sirro amesema kuwa hakuna taarifa na pia hakuna uthibitisho kuwa maandamano hayo yatapokewa na Rais Magufuli.
Pia, Kamanda Sirro alieleza kuwa BAVICHA hawakuanisha barabara ambazo wanatarajia kutumia katika maandamano hayo. 
“Siku hiyo sio nzuri sana
kwa sababu ni siku ambayo watu wanakuwa kazini. Ni siku ambayo wengi
watataka kutumia barabara hizo kwa ajili ya huduma za kijamii na kwa
sababu kuna option nyingine ya kuweza kupata suluhu hiyo, nisema tu
kwamba maandamano hayo yamepigwa marufuku,” alisema.
Post a Comment: