Thursday, 25 February 2016



Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelaumiwa na wasanii wa sanaa za uchoraji, mara baada ya wasanii hao kudai kuwa serikali hiyo haijawalipa ujira wao baada ya kazi za uchoraji picha za asili ndani ya ikulu hiyo.
IMG-20160203-WA0002
Wakizungumza na Mtembezi.com wasanii hao wamesema walipata tenda ya uchoraji michoro ya utamaduni ndani ya ikulu hiyo iliyopo  Magogoni jiini Dar es salaam.
IMG-20160201-WA0001
Mmoja wa wasanii hao wa sanaa za uchoraji anae fahamika kwa jina la Masoud Kibwana amesema  ameeleza malalamiko juu ya ucheleweshwaji wa malipo ya ya kazi zao za sanaa, ambazo zilichukuliwa kwa ajiri ya mapambo  ndani ya Ikulu hiyo ambapo amesema kazi hizo zilikusanywa tangu mwaka jana  mwezi wa 8 ikiwa ndani ya kipindi cha kampeni ambapo waliambiwa kuwa  watalipwa pesa zao kabla ya kipindi hicho kuisha.
IMG-20160131-WA0004 (1)
Aidha amesema wame shangazwa na hatua ya serikali kuwa cheleweshea fedha zao licha ya muda mrefu kupita  kinyume na makubaliano yao.
IMG-20160131-WA0005
Vilevile ameeleza kuwa kiongozi ambae   alikuwa ameshika tenda hiyo ambae amemtaja kwa jina la  George Bakelana hapatikani  kwenye simu na hata akipatikana hapokei simu zao na baada ya siku kadhaa kupita kiongozi huyo aliwapigia simu  na kuwaambia kuwa atawapa maelekezo juu ya kazi zao.
ikulu
Akieleza baadhi ya hatua walizozipitia kutatua suala hilo msanii huyo wa sanaa ya uchoraji amesema wamejitahidi kufanya ufuatiiaji  kupitia Shirikisho la Sanaa Tanzania bila mafanikio yeyote.

SOURCE : http://mtembezi.com/index.php/2016/02/25/jipu-ndani-ya-ikul

Post a Comment: