Dondoo za mkutano wa Magufuli na wazee wa Dar
∆ "Sijachangua wakuu wa Mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi ili niwapime ni nani wanatosha na wepi hawatoshi" - Mhe Rais Dkt @MagufuliJP
∆ "Wapo waandishi wanaandika mabaya tu na uchonganishi, utadhani yakitokea machafuko wana sehemu nyingine ya kuishi"- Mhe Rais Dkt @MagufuliJP
∆ "..Watanzania tujenge utamaduni wa kupenda kulipa kodi na kudai risiti.." - Mhe Rais @MagufuliJP,
∆ Nataka mjue kuwa ni watu wachache sana ambao wametufikisha hapa, tutawashughulikia kwa faida yenu. - Dkt @MagufuliJP
∆ Vyombo vya usalama viko imara kila kona, vitamshughulikia yeyote atakayechokoza. - Dkt @MagufuliJP
∆ Sijaliingilia suala la Znz na sitaliingilia, wenye malalamiko waende mahakaman ila nitahakikisha Amani na salama inapatikana nchi nzima-
∆ Tunaomba mtuvumilie tutumbue haya majipu na tutayatumbua kwelikweli, hata yakihama tutayatumbua tu. - Dkt @MagufuliJP
∆ "Barabara ya kutoka Dar es salaam mpaka Chalinze itajengwa kwa njia sita na itakuwa na fly over 7" - Mhe Rais Dkt @MagufuliJP, Dar es salaam
∆ Tarehe ya kuteua ma RC na ma DC hamtaijua lakini Makonda angalau wewe umeshajihakikishia utakuwemo. - Dkt @MagufuliJP
∆ Siingilii Zanzibar, ZEC iko huru, nitaendele kukaa kimya, ukileta fyokofyoko kazi yangu ni kuhakikisha usalama unakuwepo. - Dkt @MagufuliJP
∆ Tuna nia ya dhati ya kuibadilisha Tanzania, na katika hili lazima kuna watu wataguswa ila ni wachache. - Dkt @MagufuliJP
∆ "..Ni wasaa wa kila Mtanzania kujipima ktk siku mia 100 za Serikali ya Awamu ya Tano, umeifanyia nini Tanzania.."
∆ "..Tumejitoa kuwatumikia watanzania, na yeyote atakayejaribu kutukwamisha tutambomoa.." - Mhe Rais Dkt @MagufuliJP,
∆ Mimi ni Mtanzania nimechaguliwa na Watanzania, nitafanya kazi Tanzania, nitafia Tanzania, nitazikwa Tanzania. - Dkt @MagufuliJP
∆ Akina mama niliokuta wamelala chini Muhimbili wahamishiwe lile jengo lingine na liwekwe vitanda ndani ya siku 2. - Dkt @MagufuliJP
∆ ".wanaosema kuwa juhudi zetu za kuleta mabadiliko ya haraka ktk nchi yetu ni nguvu ya soda, wanajidanganya, hata Coca ukichanganya na Gongo utalewa TUU Tumedhamiria." - Mhe @MagufuliJP
Post a Comment: